

Lugha Nyingine
Wakulima katika pilika za kuchuma majani ya chai huko Pu'er, Mkoa wa Yunnan, China
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 20, 2023
![]() |
Mkulima wa chai akichuma majani ya chai katika msitu wa chai wa kale wa Mlima Jingmai ulioko Eneo la Pu'er katika Mkoa wa Yunnan Kusini-Magharibi mwa China, Septemba 19, 2023. (Xinhua/Tang Rufeng) |
Wakulima wenyeji wa Eneo la Pu'er katika Mkoa wa Yunnan Kusini-Magharibi mwa China wako katika pilika za kuchuma majani ya chai katika msimu wa mavuno ili kukidhi mahitaji ya soko.
Mandhari ya Kitamaduni ya Msitu wa Chai wa Kale wa Mlima Jingmai katika eneo hilo la Pu'er imeingizwa kwenye Orodha ya Mali ya Urithi ya Dunia ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) siku ya Jumapili.
Ikijumuisha misitu mitano mikubwa ya chai iliyohifadhiwa vizuri, vijiji tisa vya jadi pamoja na hifadhi za misitu mitatu, mandhari hiyo inasimama kama mfano wa utamaduni tajiri wa chai unaohusisha mila na desturi za kale za kulima na kuhifadhi misitu ya kale ya chai
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma