

Lugha Nyingine
BRI ni muhimu katika kuleta ustawi na kutoa sauti yenye nguvu kwa Nchi za Kusini, asema mtaalamu wa Uingereza
BEIJING – Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) ambalo limependekezwa na China lina maana kubwa kwani linaleta ustawi na imani kwa Nchi za Kusini na "kutoa sauti kubwa kwa wale ambao hawana sauti kwa sasa," David Ferguson, mhariri mkuu wa heshima wa Kiingereza wa Shirika la Uchapishaji la Lugha za Kigeni hapa Beijing, ambaye amekuwa akiishi na kufanya kazi nchini China kwa zaidi ya miaka 15 ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua hivi karibuni.
"BRI ni muhimu angalau kati ya idadi ndogo za mapendekezo tangu kumalizika kwa Vita vya Pili vya Dunia, kwa mfano, kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa na kusainiwa kwa Mkataba wa Paris, lakini ina umuhimu mkubwa zaidi kwamba itakuwa na mchango mkubwa kwa Dunia," Ferguson amesema.
BRI "italeta ustawi kwa nchi nyingi maskini na zinazoendelea katika kutekelezwa kwake. Itaongeza imani kwa nchi hizi katika mfumo na utamaduni ... na kimsingi itabadilisha muundo wa utaratibu wa kimataifa," amesema Ferguson ambaye alipokea Tuzo za Orchid za China mapema Mwezi Septemba kwa sababu ya kuwezesha mabadilishano ya kitamaduni kati ya China na nchi nyingine duniani.
"Siku zote imesisitiza (kwamba) nchi zote, bila kujali ni imara kiasi gani au dhaifu kiasi gani, haijalishi zina nguvu kiasi gani, kubwa au ndogo, zinapaswa kuwa na sauti sawa," ameongeza.
Kwa miaka mingi, Ferguson amehariri tafsiri ya Kiingereza ya kazi za viongozi wa China, ikiwa ni pamoja na juzuu nne za kitabu cha "Xi Jinping: Utawala wa Nchi," pamoja na nyaraka za serikali na vitabu vinavyolenga kuwasilisha mitazamo ya China kwa hadhira ya kimataifa, na ameandika mkusanyo wa vitabu vinavyotambulisha asili za kihistoria na michakato ya maendeleo ya utandawazi wa kisasa wa miji ya China.
Mtaalamu huyo amebainisha kuwa BRI imekuwa ikilengwa kwa ukosoaji na kuchafuliwa na baadhi ya nchi na vyombo vya habari vya Magharibi tangu kutangazwa kwake Mwaka 2013.
Nchi za Magharibi zimekuwa zikizungumzia kile kinachoitwa "ukoloni wa mamboleo wa China," na kile kinachojulikana kama "mitego ya madeni," lakini hiyo inatokana na kujenga hoja zenye imani na uelewa potofu, amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma