

Lugha Nyingine
Mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wafunguliwa (2)
UMOJA WA MATAIFA - Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umefunguliwa Jumanne kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, ukilenga kurejesha imani na mshikamano duniani katika wakati huu wenye changamoto.
Dennis Francis, Rais wa Kikao cha 78 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ameongoza hafla ya ufunguzi wa mjadala huo wenye mada "Kujenga upya uaminifu na kuamsha mshikamano wa kimataifa: Kuharakisha hatua za Ajenda ya 2030 na Malengo ya Maendeleo Endelevu kuelekea amani, ustawi, maendeleo na uendelevu kwa wote."
Kwenye hotuba yake ya ufunguzi, Francis amesisitiza umuhimu wa kuunganisha nchi zote ili kukabiliana na changamoto za kimataifa.
"Mwaka huu, jukumu letu liko wazi: kuunganisha nchi, ili kuwa na umoja katika kuamini madhumuni ya pamoja na kuwa katika mshikamano katika hatua za pamoja," amesema.
Amesema Dunia ina uwezo wa kuleta mabadiliko iwapo kuna nia ya kuchukua hatua.
“Njia ya pamoja iliyoratibiwa inahitajika sasa, sana zaidi kuliko wakati wowote katika historia. Vita, mabadiliko ya tabianchi, madeni, nishati na majanga ya chakula, umaskini na njaa. Misukosuko hiyo inaathiri moja kwa moja maisha na ustawi wa mabilioni ya watu kote duniani. Zinarudisha nyuma mafanikio ya maendeleo yaliyopatikana kwa bidii miongo kadhaa iliyopita, na hivyo kuwafanya mamilioni ya watu waishi na umaskini na ugumu vizazi kwa vizazi,” amesema.
Amesema, wakati baadhi ya mafanikio yamefikiwa kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), Mkutano wa Kilele wa SDG unaitishwa pembezoni mwa Mjadala Mkuu katika muktadha ambapo kumekuwa na kuchelewa na kurudi nyuma kwa malengo hayo kusikokubalika.
Kwenye ripoti yake ya "hali ya Dunia" kabla ya kufunguliwa kwa Mjadala Mkuu wa mwaka huu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kuanzisha taasisi za kimataifa za ushirikiano wa pande nyingi ili kukabiliana na changamoto za kimataifa.
Guterres ameonya kwamba Dunia inazidi kuyumba, akitaja masuala kama vile mivutano ya siasa za kijiografia, athari za mabadiliko ya tabianchi, teknolojia vurugishi na mabadiliko ya dunia yenye machafuko.
Ametoa wito wa dhamira ya kushikilia ahadi ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya amani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma