

Lugha Nyingine
Mandhari nzuri ya mavuno ya majira ya kiangazi vijijini katika Mji wa Xinfeng, Mkoa wa Jiangxi, China
![]() |
Wanakijiji wakiendesha mashine za kuvuna mazao shambani kwa ajili ya kuvuna mpunga katika Wilaya ya Xinfeng iliyoko Mkoa wa Jiangxi, Kusini Mashariki mwa China, Septemba 19. (Xinhua/Zhu Haipeng) |
Ganzhou, China - Hivi karibuni, Wanakijiji katika Kijiji cha Huangtian kilichoko Kitongoji cha Xinfeng, Mji wa Ganzhou,Mkoa wa Jiangxi, Kusini Mashariki mwa China waliendesha mashine za kuvuna mazao shambani kwa ajili kuvuna mpunga wa saizi ya kati.
Katika siku za hivi karibuni, mpunga uliopandwa katika vijiji vya Wilaya ya Xinfeng katika Mkoa wa Jiangxi, Kusini Mashariki mwa China umebadilika rangi kutoka rangi ya kijani kuwa njano. Wanakijiji wanachukua fursa nzuri ya hali ya hewa nzuri kuvuna na kukausha mpunga wao, na kutengeneza mandhari ya mavuno mengi. Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya eneo hilo imeongeza ruzuku kwa ajili ya kununua zana za kilimo, ikihamasisha wanakijiji kikamilifu kutumia mfumo wa kisasa wa kupanda mbegu, upandikizaji na utapanyaji miche kwa kutumia mashine, na kuvuna kwa kutumia mashine. Kupitia muundo wa "kampuni + ushirika + wakulima" imesababisha kuongezeka kwa ubora na tija ya upandaji nafaka, kusaidia kuongeza uzalishaji wa mazao na kipato."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma