

Lugha Nyingine
Maonyesho ya Viwanda ya Dunia Mwaka 2023 yaangazia utengenezaji bidhaa kwa kutumia teknolojia za akili bandia (5)
![]() |
Picha iliyopigwa Septemba 20, 2023 ikionyesha hafla ya ufunguzi wa Maonyesho ya Viwanda ya Dunia Mwaka 2023 huko Hefei, Mkoa wa Anhui, Mashariki mwa China, Septemba 20, 2023. (Xinhua/Zhou Mu) |
HEFEI - Maonyesho ya Viwanda ya Dunia Mwaka 2023 yameanza siku ya Jumatano huko Hefei, Mji Mkuu wa Mkoa wa Anhui, Mashariki mwa China, yakiangazia kaulimbiu ya "Viwanda vya kutumia teknolojia za akili bandia kwa mustakabali bora wa siku zijazo."
Yakiwa na idadi ya kuvunja rekodi ya kampuni zinazoonyesha bidhaa, maonyesho hayo yatakayofanyika kwa siku tano yanahusisha shughuli kama vile maonyesho, mikutano ya kilele na mikutano ya baraza.
Wageni zaidi ya 1,200 kutoka ndani na nje ya China watahudhuria maonyesho hayo, wakiwemo mabalozi na wanadiplomasia 20 wa kigeni.
Siku ya Jumanne, mabalozi na wanadiplomasia hao walitembelea baadhi ya kampuni za huko Hefei, ikiwa ni pamoja na kampuni ya kuunda magari yanayotumia nishati ya umeme ya NIO na iFLYTEK, ambayo ni kampuni ya teknolojia za akili bandia (AI) na za kuwezesha uwasilishaji hotuba inayoongoza nchini China.
"Utengenezaji bidhaa ni muhimu sana kwa nchi zinazoendelea," amesema Siyabonga C. Cwele, Balozi wa Afrika Kusini nchini China, alipotembelea NIO, huku akiongeza kuwa China imekuwa mji mkuu wa viwanda duniani na imekuwa kiongozi kwa sababu inakwenda na wakati.
Yakichukua eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 80,000, maonyesho hayo ya mwaka huu yataonyesha teknolojia mbalimbali za kisasa, zikiwemo kompyuta za quantum, roketi, magari yanayotumia nishati mpya na treni za maglev zenye kasi ya juu zaidi ya kilomita 600 kwa saa.
Kivutio kingine cha maonyesho hayo ni kwamba umeme wote utakaotumika wakati wa shughuli hizo utakuwa nishati safi kwa asilimia 100 itakayonunuliwa kupitia utaratibu wa biashara ya umeme bila kutoa uchafuzi kwa mazingira. Pia ni mara ya kwanza kwa shughuli kuu inayofanyika Anhui kutumia nishati safi katika mchakato wake wote.
Yakiwa yamefanyika tangu Mwaka 2018, Maonyesho ya Viwanda ya Dunia yamevutia zaidi ya washiriki 14,800. Jumla ya miradi 3,021 imetiwa saini, huku uwekezaji halisi ukizidi Yuan trilioni 1 (karibu dola za Kimarekani bilioni 139.4).
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma