Hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi kwenye Mradi wa Bandari ya Uvuvi ya Kilwa, Tanzania unaojengwa na Kampuni ya China yafanyika (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 21, 2023
Hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi kwenye Mradi wa Bandari ya Uvuvi ya Kilwa, Tanzania unaojengwa na Kampuni ya China yafanyika
Picha ikionesha hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi na uzinduzi wa ujenzi wa mradi wa bandari ya uvuvi ya Kilwa, Tanzania. (Picha kwa hisani ya Kampuni ya Bandari ya China)

Hafla ya uwekaji jiwe la msingi na uzinduzi wa ujenzi wa mradi wa bandari ya uvuvi ya Kilwa katika Mkoa wa Lindi nchini Tazania unaojengwa na Kampuni ya Bandari ya China (CHEC) imefanyika Jumanne, Tarehe 19, Septemba. Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania alihudhuria shughuli hiyo pamoja na waziri wa uvuvi, katibu mkuu , waziri wa uchukuzi na mkuu wa mkoa wa Lindi na maofisa wengine wa serikali.

Rais Samia amesifu sana hali ya utekelezaji na kasi ya maendeleo ya ujenzi wa mradi huo, huku akisisitiza kuwa mradi wa bandari hiyo unahusiana na uchumi wa mkoa na maisha ya watu wa Lindi na wa taifa zima la Tanzania. Ametaka pande zote husika zishirikiane vizuri, na serikali ya mkoa itoe uungaji mkono ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati uliopangwa.

Mradi wa Bandari ya Uvuvi ya Kilwa ni bandari ya kwanza ya uvuvi ya kisasa ya Tanzania, ikiwa na usanifu wa uwezo wa kupakuwa samaki tani 60,000 kila mwaka. Ni mradi kinara katika mpango wa tatu wa maendeleo ya miaka tano wa nchi hiyo.

Xu Xinpei, Meneja wa Kampuni ya Bandari ya China tawi la Afrika ya Mashariki amesema, tangu ujenzi wa mradi huo ulipoanza mwezi Februari, 2023, kazi za maandalizi, kama vile kupeleka wafanyakazi na mashine na vifaa zimekamilika kwa mafanikio. Hadi hivi sasa ujenzi wa msingi, usanifu wa awali wa gati na hatua nyingine kadha wa kadha za ujenzi wa mradi zimeanza kikamilifu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha