Ushirikiano wa kilimo kati ya Kenya na China wasaidia mapambano dhidi ya njaa, mabadiliko ya vijijini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 21, 2023
Ushirikiano wa kilimo kati ya Kenya na China wasaidia mapambano dhidi ya njaa, mabadiliko ya vijijini
Mwanafunzi wa shahada ya uzamili wa Kenya akifanya majaribio katika Maabara ya Pamoja ya Ukanda Mmoja, Njia Moja ya China na Kenya kuhusu Biolojia ya Molekuli ya Mazao katika Chuo Kikuu cha Egerton katika Kaunti ya Nakuru, Kenya, Septemba 18, 2023. (Xinhua/Han Xu)

NAIROBI - Akiwa na uso wa ng’aavu wenye kutabasamu, Hannah Wanjiku aliongoza wageni ndani ya shamba lake, lililo kwenye ukingo wa mlima wenye misitu katika eneo la Bonde la Ufa, Kaunti ya Nakuru, nchini Kenya ili kutazama mazao ya chakula yanayochanua, ikiwa ni pamoja na mahindi, maharangwe na mboga.

Karibu na nyumba ya familia ya Wanjiku, kibanda cha kilimo cha kisasa kilichogeuzwa kuwa shamba la kielelezo la muda kimevutia wakulima wadogo wa eneo hilo wanaotaka kujifunza kuhusu kilimo cha aina za nyanya zinazotoa mazao mengi.

Mwalimu huyo mstaafu ni mnufaika wa mradi wa utafiti wa ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Egerton cha Kenya na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Nanjing cha China ambao umeharakisha maendeleo ya mazao yanayostahimili wadudu, ukame na magonjwa ili kukabiliana na njaa, utapiamlo na umaskini vijijini.

"Tunatarajia kupata teknolojia mpya za kilimo kutoka China ili kusaidia kuongeza mavuno ya mazao na kushughulikia changamoto zinazowakabili wakulima wenyeji kama vile mvua zisizokuwa na uhakika, gharama ya juu ya mbolea na mbegu," Wanjiku ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua siku ya Jumatatu akiwa kwenye shamba lake.

Ukiwa umeanza katika miaka ya 1990, ushirikiano kati ya vyuo vikuu hivyo viwili umejikita katika utafiti wa mazao mseto pamoja na mafunzo kwa wakulima na wahudumu kuhusu mbinu bora za kilimo, amesema Richard Mulwa, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Egerton.

Mulwa ameitaja Maabara ya Pamoja ya Ukanda Mmoja, Njia Moja ya China na Kenya kuhusu Biolojia ya Molekuli ya Mazao, inayomilikiwa na Chuo Kikuu cha Egerton, kwa kufanya kazi kama kituo muhimu cha utafiti na uhimizaji wa mazao yenye mavuno mengi kupitia teknolojia na utaalamu kutoka China.

Mulwa amesema maabara hiyo ya kisasa, ambayo ilizinduliwa Jumatatu, inatarajiwa kuwezesha utafiti wa msingi, kuzaliana kwa mazao, na kutolewa kwa mazao ambayo yanaweza kuhimili mabadiliko ya tabianchi.

Kwa mujibu wa Mulwa, maabara hiyo pia itatumika kama "kituo cha neva" cha ujuzi na uhamishaji wa teknolojia, ukiacha kutoa mafunzo kwa wataalam kutoka ukanda wa Afrika Mashariki juu ya kuzalisha miche na mbegu za mazao ya chakula yanayostahimili tabianchi.

Mulwa anasema kuwa, ushirikiano wa kilimo kati ya Kenya na China, umehakikisha kwamba wakulima wadogo wanapata teknolojia na mbegu bora na kuimarisha usalama wa chakula na mapato ya kaya.

Wajumbe kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Nanjing walishuhudia uzinduzi wa Maabara ya Pamoja ya Ukanda Mmoja, Njia Moja ya China na Kenya kuhusu Biolojia ya Molekuli ya Mazao.

Ili kuendeleza utafiti na uvumbuzi wa kilimo nchini Kenya na nchi jirani, vifaa vya kisasa vya maabara ya kielelezo viliwekwa kwa fedha kutoka kwa serikali ya China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha