Rais Xi Jinping wa China afanya ziara ya ukaguzi katika Mji wa Yiwu mkoani Zhejiang

(CRI Online) Septemba 22, 2023
Rais Xi Jinping wa China afanya ziara ya ukaguzi katika Mji wa Yiwu mkoani Zhejiang
(Picha inatoka Shirika la Habari la China Xinhua.)

Rais wa China Xi Jinping amefanya ziara ya ukaguzi katika Mji wa Yiwu mkoani Zhejiang.

Katika ziara yake hiyo, Rais Xi ametembelea soko la biashara ya kimataifa la Yiwu ambalo ni soko kubwa zaidi duniani la kuuza bidhaa ndogo ndogo kwa bei ya jumla na kutoa ajira kwa watu milioni 32. Mwaka jana, thamani ya jumla ya miamala katika soko hilo ilizidi yuan bilioni 200.

Rais Xi pia ametembelea Kijiji cha Lizu cha mji huo ambacho kina familia 333 na kwa jumla watu 706. Miaka ya hivi karibuni, kutokana na kutekelezwa kwa kina mikakati ya “ustawishaji vijijini” na kuimarishwa kwa kiwango cha miundombinu, mapato ya wastani ya kila mwanakijiji katika kijiji hicho yameongezeka kwa yuan 2,500 kila mwezi, na idadi ya watalii wanaotembelea kijiji hicho imefikia zaidi ya laki 2 kila mwaka.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha