Katibu Mkuu wa UN atoa wito wa kuwepo kwa ushirikiano wa pande nyingi unaoendana na Dunia yenye nchi nyingi zenye nguvu sawa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 22, 2023
Katibu Mkuu wa UN atoa wito wa kuwepo kwa ushirikiano wa pande nyingi unaoendana na Dunia yenye nchi nyingi zenye nguvu sawa
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza katika mkutano wa maandalizi wa mawaziri ya Mkutano wa Kilele kuhusu Siku za Baadaye kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Septemba 21, 2023. (Xinhua/Li Rui)

UMOJA WA MATAIFA - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres siku ya Alhamisi amesisitiza umuhimu wa taasisi za ushirikiano wa pande nyingi ambazo zinaendana na hali ya Dunia kuwa na nchi nyingi zenye nguvu sawa ambayo inaendelea kujengwa.

"Tunaelekea kwenye hali ya Dunia kuwa na nchi nyingi zenye nguvu sawa. Kuwa na nchi nyingi zenye nguvu sawa kunatengeneza fursa mpya kwa nchi mbalimbali kuongoza katika ngazi ya kimataifa. Lakini historia inafundisha kwamba kuwa na nchi nyingi zenye nguvu sawa bila taasisi zenye nguvu za ushirikiano wa pande nyingi huleta hatari kubwa. Inaweza kusababisha mvutano mkubwa zaidi wa siasa za kijiografia, ushindani wenye vurugu na zaidi kugawanyika," amesema kwenye mkutano wa maandizi wa mawaziri ya Mkutano wa Kilele kuhusu Siku za Baadaye.

Amesema, taasisi za ushirikiano wa pande nyingi zitadumu tu ikiwa ziko duniani kote. Mkutano wa Kilele kuhusu Siku za Baadaye wa mwaka ujao ni fursa ya kipekee ya kusaidia kujenga upya uaminifu na kuzifanya taasisi na mifumo kazi ya ushirikiano wa pande nyingi iliyopitwa na wakati ili kuendana na Dunia ya sasa, kwa kuzingatia usawa na mshikamano.

Ameongeza kuwa, mkutano huo ni zaidi ya fursa. Ni njia muhimu ya kupunguza hatari na kujenga Dunia salama na yenye amani zaidi.

Guterres amekaribisha nchi wanachama kukubaliana kupitisha Mkataba kwa ajili ya Siku za Baadaye uliojadiliwa baina serikali katika Mkutano huo, kufufua Mkataba wa Umoja wa Mataifa, kuimarisha ushirikiano wa pande nyingi, kuimarisha utekelezaji wa ahadi zilizopo, na kukubaliana juu ya ufumbuzi wa changamoto mpya.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha