Nchi za Pembe ya Afrika zataka hatua zichukuliwe dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, kugeuza mfumo wa kimataifa (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 25, 2023
Nchi za Pembe ya Afrika zataka hatua zichukuliwe dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, kugeuza mfumo wa kimataifa
Mahamoud Ali Youssouf (kwenye jukwaa na kwenye skrini), Waziri wa Mambo ya Nje wa Djibouti, akitoa hotuba katika Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Septemba 23, 2023. (Xinhua) /Li Rui)

UMOJA WA MATAIFA – Kwenye Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, nchi za Pembe ya Afrika zimetoa wito kwa shauku kuchukuliwa hatua ili kukabiliana na tishio la mabadiliko ya tabianchi na kuufanyia mageuzi mfumo kazi wa sasa wa kifedha wa kimataifa uliopitwa na wakati na usio wa haki.

Viongozi kutoka Somalia, Ethiopia, Djibouti na Eritrea kwa wakati tofauti siku ya Jumamosi wakitoa hotuba zao wameonyesha hali mbaya ya Dunia iliyoathiriwa sana na mabadiliko ya tabianchi. Ujumbe wao haukuwa na shaka: Janga hili kubwa linahitaji juhudi za haraka na za pamoja.

Hamza Abdi Barre, Waziri Mkuu wa Somalia, amesisitiza "nguvu ya mshikamano na ushirikiano" katika Dunia iliyounganishwa na kuwataka viongozi kuharakisha uchukuaji hatua ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu wa Ethiopia Demeke Mekonnen Hassen amewauliza viongozi wa Dunia: "Je, tunayo nia muhimu ya kisiasa ya kuchagua ushirikiano wa kimataifa badala ya ushindani wa siasa za kijiografia (na) je, tumejiandaa kufanya kazi pamoja kuelekea zama yenye mustakabali mzuri wa ustawi wa pamoja?"

Hassen ameelezea ukweli mchungu kwamba maamuzi ya sasa ya sera yanazidisha mivutano, huku umaskini na njaa vikiongezeka na SDGs kudhoofishwa.

Kuhusu usalama wa kimataifa, kiongozi huyo kutoka Ethiopia amesisitiza umuhimu wa mfumo unaoheshimu uhuru wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na kuzuia migogoro.

"Kufanyia mageuzi Baraza la Usalama siyo chaguo lakini ni lazima kabisa," amesisitiza, huku akitoa wito wa kuwepo kwa ujumbe wa kudumu kwa Afrika.

Mahamoud Ali Youssouf, Waziri wa Mambo ya Nje wa Djibouti, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa pande nyingi na ushirikiano wa kimataifa.

Kuna tabia ya "kujikusanya pamoja katika vilabu," Youssouf amesema, akiongeza kuwa "ushirikiano wa pande chache" (minilateralism) huu unasababisha upinzani wa mageuzi katika taasisi za kimataifa, na hivyo kufanya hali ya ukosefu wa usawa duniani kuzidi kuwa mbaya na kuongeza ushindani wa siasa za kijiografia.

Osman Saleh Mohammed, Waziri wa Mambo ya Nje wa Eritrea, amesisitiza kwamba Umoja wa Mataifa unahitaji kuboresha muundo na mamlaka yake ili kutimiza malengo yake ya kihistoria.

Amesisitiza kuwa kulifanyia mageuzi Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa haipaswi kuwa tu kupanua uanachama.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha