Mkutano wa kubadilishana uzoefu wa kuboresha mazingira ya biashara 2023 wafanyika Erdos, Mongolia ya Ndani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 26, 2023
Mkutano wa kubadilishana uzoefu wa kuboresha mazingira ya biashara 2023 wafanyika Erdos, Mongolia ya Ndani
(Picha ilipigwa na Liu Yilin/People's Daily Online)

Chini ya maandalizi ya pamoja ya People’s Daily Online, Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani na serikali ya mji wa Erdos, Mkutano wa kubadilishana uzoefu wa kuboresha mazingira ya biashara 2023 umefanyika tarehe 22, Septemba huko Erdos, Mongolia ya Ndani, China. Viongozi husika, wasomi na wataalam wa sekta ya mazingira ya biashara kutoka sehemu mbalimbali nchini China walishiriki kwenye mkutano huo.

Mkuu wa Shirika la Uchambuzi wa Sera la China Ma Li, ambaye pia ni naibu mhariri mkuu wa zamani wa gazeti maarufu la China, People’s Daily, mtendaji mkuu na rais wa kampuni ya People’s Daily Online Ye Zhenzhen, naibu mkurugenzi mtendaji wa Ofisi ya Uenezi ya Kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ya Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani Fu Lei, ambaye pia ni mkuu wa Idara ya Uchapishaji na Habari ya mkoa huo walihudhuria mkutano huo.

Mazingira ya biashara yanahusiana moja kwa moja na shauku na ari ya wadau wa biashara, kwa hivyo yana umuhimu mkubwa katika kuongeza uhai wa uchumi na msukumo wa ongezeko la uchumi.

Katika miaka ya hivi karibuni, Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani umepata maendeleo makubwa katika kuboresha mazingira ya biashara. Mchakato mzima wa uidhinishaji wa vibali vya miradi hutekelezwa mtandaoni, kiwango cha kushughulikia maombi ya vibali mtandaoni kimefikia asilimia 83.6 kwenye mkoa mzima; mfumo wa “mtandaoni + ukaguzi” umeboreshwa. Serikali ya mkoa ilianzisha kampeni ya kuondoa vitendo vya ukosefu wa uaminifu na kulipa deni lenye thamani ya Yuan zaidi ya bilioni 110 (takriban Dola za Kimarekani bilioni 15) linalodaiwa na kampuni ndogo na za kati.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha