Michezo ya Asia ya Hangzhou yafungwa rasmi ikiwa na "mafanikio ambayo hayajawahi kutokea" (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 09, 2023
Michezo ya Asia ya Hangzhou yafungwa rasmi ikiwa na
Wacheza ngoma wakiwa wamejaza uwanja kushiriki kwenye hafla ya kufunga Michezo ya Asia ya Hangzhou. (Xinhua/Meng Chenguang)

HANGZHOU – Hafla ya kufunga Michezo ya 19 ya Asia umefanyika hapa siku ya Jumapili chini ya kaulimbiu isemayo "Kumbukumbu za Kudumu za Hangzhou", ikiangazia nguvu na umoja wa michezo na Michezo ya Asia.

Katika siku 16 zilizopita, wanamichezo wapatao 12,000 kutoka nchi na maeneo 45 walishiriki nyakati nzuri zisizosahaulika huko Hangzhou, ikiwa ni mara ya tatu kwa China kuwa mwenyeji wa michezo hiyo, baada ya Beijing kuandaa Mwaka 1990 na Guangzhou Mwaka 2010.

Huku michezo ya dansi ya kunyumbua viungo na michezo ya kidijitali ikijitokeza kwa mara ya kwanza kuwa michezo rasmi ya kushindaniwa medali, Michezo ya Asia ya Hangzhou ilihusisha michezo 40, ya aina 61 na shughuli 481. China imejinyakulia medali za dhahabu 201, fedha 111 na shaba 71, na kuwepo kileleni mwa orodha ya medali kwa awamu 11 mfululizo za Michezo ya Asia tangu Mwaka 1982 na kuboresha rekodi yake ya hapo awali ya kunyakua medali za dhahabu 199 huko Guangzhou Mwaka 2010.

Waziri Mkuu wa China Li Qiang na Kaimu Rais wa Baraza la Olimpiki la Asia (OCA) Raja Randhir Singh walihudhuria hafla ya kufunga kwenye Kituo cha Michezo ya Olimpiki cha Hangzhou.

Singh ametangaza kuwa Michezo ya Asia imefungwa, akiisifu China ni "mwenyeji kamili ambaye OCA haitamsahau kamwe."

"Nguvu ya michezo, nguvu ya Michezo ya Asia ni kutuunganisha sote maishani. Napenda kuishukuru serikali ya China, Kamati ya Olimpiki ya China, watu wa Hangzhou na kamati ya maandalizi ya Hangzhou (HAGOC) kwa haya mliyofanya na kuhakikisha kuwa Michezo ya Asia ya Hangzhou inakuwa yenye mafanikio ambayo hayajawahi kutokea," Singh amesema.

Xie Zhenye, ambaye alipata ushindi mara mbili wa medali za dhahabu katika mbio za mita 100 na zile za 4x100 za kupokezana vijiti kwa wanaume huko Hangzhou, amekuwa mshika bendera wa ujumbe wa wanamichezo wa China kwenye hafla hiyo ya kufunga.

Wakibadilika kutoka kuwa watazamaji hadi washiriki, wanamichezo walitembea hadi uwanjani, huku kukiwa na muundo wa ukumbi wa maonyesho ya jukwaani na vifaa vya sanaa ya Bustani ya Asia.

Huku bendera ya OCA ikishushwa na wimbo wa OCA kuchezwa, meya wa Mji wa Hangzhou Yao Gaoyuan alimkabidhi Singh bendera, ambaye baadaye aliikabidhi kwa Hideaki Omura, gavana wa Mkoa wa Aichi na Hideo Nakata, Naibu Meya wa Mji wa Nagoya wa Japan, mji ambao utakuwa mwenyeji wa Michezo ya Asia ya Mwaka 2026.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha