Picha: Ujenzi wa bandari mbalimbali katika miaka 10 tangu Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” litolewe waleta fursa mpya za ushirikiano

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 09, 2023
Picha: Ujenzi wa bandari mbalimbali katika miaka 10 tangu Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” litolewe waleta fursa mpya za ushirikiano
Meli ya mizigo ikitia nanga kwenye gati la bandari ya Doraleh huko Djibouti, Mji Mkuu wa Djibouti Tarehe 20, Septemba, 2022. (Picha na Dong Jianghui/Shirika la Habari la China, Xinhua)

Oktoba 3, 2013, China ilitoa pendekezo la kujenga kwa pamoja Njia ya Hariri ya Baharini ya Karne ya 21. Pendekezo hilo pamoja na lile la Ukanda wa Kiuchumi wa Njia ya Hariri, lililotolewa na China mwaka huo huo yameunda “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, na kufungua ukurasa mpya katika ushirikiano wa kimataifa. Katika mwongo uliopita, pendekezo la kujenga pamoja Ukanda Mmoja, Njia Moja limeleta simulizi nyingi zaidi kuhusu ustawi wa pamoja kwenye bahari ya buluu. Bandari mbalimbali mpya zimejengwa na kukamilika moja baada ya nyingine, zikitoa fursa mpya za ushirikiano.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha