Israel yaizingira Gaza huku kukiwa na mgogoro unaoongezeka na Hamas, mashambulizi kwenye mpaka na Lebanon (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 10, 2023
Israel yaizingira Gaza huku kukiwa na mgogoro unaoongezeka na Hamas, mashambulizi kwenye mpaka na Lebanon
Mtu akiangalia majengo yaliyobomolewa kufuatia shambulizi la anga la Israel katika Mji wa Gaza, Oktoba 8, 2023. (Picha na Rizek Abdeljawad/Xinhua)

JERUSALEM/GAZA - Israel imeongeza mashambulizi yake ya anga huko Gaza siku ya Jumatatu na kutangaza amri ya "kudhibiti kikamilifu" eneo la Palestina katika siku ya tatu ya mgogoro kufuatia mashambulizi ya ghafla yaliyofanywa na Kundi la Hamas dhidi ya Israel Jumamosi huku idadi ya vifo na majeruhi kutokana na mashambulizi ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza ikiongezeka hadi 687 na 3,726, mtawalia, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya ya Palestina siku ya Jumatatu.

Idadi ya waliofariki kutokana na mashambulizi ya kushtukiza ya Hamas mwishoni mwa wiki Kusini mwa Israel imeongezeka hadi zaidi ya 900, televisheni inayomilikiwa na serikali ya Israel ya Kan imeripoti Jumatatu. Idadi ya watu waliojeruhiwa waliopokelewa na hospitali imeongezeka hadi kufikia 2,616, ikiwa ni pamoja na 25 walio katika hali mbaya, Wizara ya Afya ya Israeli imeeleza katika taarifa mpya.

"Nimeamuru kubadili mbinu (kutoka ulinzi) hadi mashambulizi makubwa ya kiwango ambacho hakijawahi kutokea," Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema katika hotuba yake kwa taifa siku ya Jumatatu.

Mapema asubuhi, Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) Daniel Hagari aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano kwamba jeshi limepata tena udhibiti wa jamii zote za makazi za Kusini mwa Israeli, ambazo zilivamiwa na wanamgambo wa Hamas siku ya Jumamosi baada ya kuvunja uzio wa usalama kati ya Israeli na Gaza.

Vikosi vya Al-Qassam, ambalo ni tawi la kijeshi la Hamas, baadaye vilisema kuwa mashambulizi ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza yamesababisha vifo vya wafungwa 4 wa Israel na mateka wanaowashikilia.

Jana Jumatatu usiku, Waziri wa Nishati wa Israel Israel Katz alitangaza kwamba "mabomba yote ya kusambaza maji kutoka Israel hadi Ukanda wa Gaza yamefungwa." Israel pia imesitisha upitishaji wa bidhaa, umeme na chakula kwenye Ukanda huo.

Kwa kujibu vitisho vya Israel, msemaji wa mrengo wa kijeshi wa Hamas Abu Obeida ameonya katika taarifa ya sauti kwamba "ulengaji wowote wa watu wetu nyumbani kwao bila ya tahadhari ya awali kwa masikitiko utakabiliwa na kunyonga mtu mmoja miongoni mwa mateka ya raia tunaowashikilia."

Makundi ya wapiganaji wa Gaza yamesema mateka wapatao 130 bado wanaendelea kushikiliwa Gaza, wakiwemo makumi ya watu wenye uraia wa nchi mbili. Thailand imethibitisha kuwa raia 11 wa Thailand wanazuiliwa na Hamas.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imetangaza Jumatatu kuwa "familia zaidi ya 17,500, ikiwa ni pamoja na watu zaidi ya 123,538, wamekimbia makazi yao."

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha