Rais Xi Jinping asisitiza maendeleo yenye ubora wa juu ya Ukanda wa Kiuchumi wa Mto Changjiang

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 13, 2023
Rais Xi Jinping asisitiza maendeleo yenye ubora wa juu ya Ukanda wa Kiuchumi wa Mto Changjiang
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) akiongoza na kutoa hotuba muhimu kwenye kongamano la kuendeleza ukanda wa kiuchumi wa Mto Changjiang huko Nanchang, Mkoa wa Jiangxi, Mashariki mwa China, Oktoba 12, 2023. (Xinhua/Ju Peng)

NANCHANG - Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) ametoa wito wa kuhimiza maendeleo yenye ubora wa juu ya Ukanda wa Kiuchumi wa Mto ili kuunga mkono na kuhudumia vizuri zaidi ujenzi wa mambo ya kisasa ya China.

Rais Xi, amesema hayo siku ya Alhamisi kwenye kongamano aliloongoza la kuendeleza maendeleo ya Ukanda wa Kiuchumi wa Mto Changjiang.

Amesisitiza umuhimu wa kutekeleza kikamilifu na kwa uaminifu dhana mpya ya maendeleo katika mambo yote, kuweka kipaumbele cha juu katika maendeleo ya kiuchumi yanayotilia maanani uhifadhi wa mazingira na kufuata maendeleo ya kijani.

Rais Xi amesema maendeleo ya eneo hilo yanapaswa kuongozwa na uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia huku ulinzi wa kiikolojia na mazingira na maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanapaswa kuendelezwa kwa uratibu mzuri.

“Pia ni muhimu kufanya uratibu wa sera na uratibu wa kazi ili kuweka mipango ya muda mrefu, kutafuta ufumbuzi wa muda mrefu na kuweka msingi wa utulivu wa kudumu,” ameongeza.

Rais Xi amesema mabadiliko yenye mafanikio ya ajabu yamefanywa katika eneo hilo katika miaka minane iliyopita tangu kutekelezwa kwa mkakati wa maendeleo ya Ukanda wa Kiuchumi wa Mto Changjiang, na mafanikio hayo yamegeuka kuwa makubaliano ya wote kuhimiza uhifadhi wa mazingira ulioratibiwa vyema na kuepuka kuhuisha kwa kupita kiasi.

Amezitaka serikali za mitaa katika eneo hilo kuendeleza mageuzi makubwa katika maeneo muhimu, kuongoza kampuni na mashirika ya kijamii ili kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Ukanda wa Kiuchumi wa Mto Changjiang, na kuhamasisha kikamilifu juhudi za watu za hiari na ubunifu wa watu.

Kongamano hilo lilihudhuriwa na Waziri Mkuu wa China Li Qiang, Mkurugenzi wa Ofisi Kuu ya Kamati Kuu ya Chama Cai Qi , na Naibu Waziri Mkuu Ding Xuexiang. Wote ni wajumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha