Bandari ya Qinzhou Kusni mwa China: kituo muhimu cha kisasa cha kimataifa kando ya ukanda wa biashara ya nchi kavu na majini (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 13, 2023
Bandari ya Qinzhou Kusni mwa China: kituo muhimu cha kisasa cha kimataifa kando ya ukanda wa biashara ya nchi kavu na majini
Picha hii ya kuunganisha ikionyesha gati la usafirishaji nishati inayojengwa Julai 24, 1997, (juu) na mandhari ya angani ya gati la usafirishaji wa nishati Agosti 28, 2022, (chini, picha iliyopigwa na mpiga picha wa Xinhua Zhang Ailin) katika Bandari ya Qinzhou huko Qinzhou, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, Kusini mwa China. (Xinhua)

Ikiwa ilianza kama kijiji kidogo cha wavuvi Mwaka 1992, Bandari ya Qinzhou katika Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, Kusini mwa China imejengwa kuwa kituo cha kisasa cha kimataifa kando ya Ukanda Mpya wa Biashara wa Nchi kavu na Majini baada ya miaka 30 ya maendeleo. Kituo cha kontena cha kiotomatiki kwa ajili ya huduma za muunganisho wa reli na bahari kimejengwa katika Bandari hiyo, pamoja na nguzo ya viwanda inayostawi katika Eneo la Majaribio la Biashara Huria la China (Guangxi) la Bandari ya Qinzhou.

Kwa sasa, Bandari ya Qinzhou imeshuhudia uendeshaji wa kila siku wa treni za kontena na kuendeleza muunganisho wake na treni za mizigo za usafiri wa China-Ulaya. Imefungua zaidi ya njia 60 za kontena za ndani na nje ya China, ambazo hufikia miji 61 nchini China na kufikia bandari 393 katika nchi na maeneo 119 duniani kote, kwa ajili ya usafirishaji wa bidhaa zaidi ya aina 940.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha