Mkutano wa Vifaa vya Baharini vya Dunia wafunguliwa katika Mkoa wa Fujian, Mashariki mwa China (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 13, 2023
Mkutano wa Vifaa vya Baharini vya Dunia wafunguliwa katika Mkoa wa Fujian, Mashariki mwa China
Picha hii iliyopigwa Oktoba 12, 2023 ikionyesha hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Vifaa vya Baharini vya Dunia 2023 huko Fuzhou, Mkoa wa Fujian, Kusini Mashariki mwa China. (Xinhua/Jiang Kehong)

FUZHOU – Mkutano wa Vifaa vya Baharini vya Dunia Mwaka 2023 umeanza Alhamisi huko Fuzhou, Mkoa wa Fujian, Mashariki mwa China, ukilenga kukusanya hekima katika sekta zikiwemo uvumbuzi wa kiteknolojia, utengenezaji wa vifaa na ushirikiano wa kiviwanda.

Shughuli hiyo itakayofanyika kwa siku nne, iliyoandaliwa kwa pamoja na Serikali ya Mkoa wa Fujian, Wizara ya Viwanda na Upashanaji wa Habari ya China na Wizara ya Uchukuzi ya China, ina kaulimbiu isemayo "Kubeba Ndoto za Binadamu kwenye Upeo Mpya katika Dunia." Inatafuta kutoa jukwaa la kiwango cha juu la mawasiliano na ushirikiano wa kimataifa katika viwanda vya vifaa vya baharini.

Mijadala sita yenye mada kuhusu teknolojia ya ujenzi wa meli barani Asia, ujenzi wa bandari ya kina kirefu ya kimataifa, na ustaarabu wa baharini wa kimataifa pia imepangwa kufanyika wakati wa shughuli hiyo.

Aidha, bidhaa, teknolojia na mipango ya utekelezaji katika nyanja ya vifaa vya baharini vilivyotengenezwa na China katika muongo mmoja uliopita zitaonyeshwa wakati wa maonyesho ya shughuli hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha