Mkutano wa Kimataifa wa Viwanda vinavyotumia Intaneti Mwaka 2023 wafunguliwa Shenyang, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 19, 2023
Mkutano wa Kimataifa wa Viwanda vinavyotumia Intaneti Mwaka 2023 wafunguliwa Shenyang, China
Washiriki wakipata uzoefu wa miwani ya uhalisia pepe (VR) ya viwandani katika Mkutano wa Kimataifa wa Viwanda vinavyotumia Intaneti Mwaka 2023, huko Shenyang, Mkoa wa Liaoning, China, Oktoba 18.

Mkutano wa Kimataifa wa Viwanda vinavyotumia Intaneti Mwaka 2023 umefunguliwa Shenyang, Mji Mkuu wa Mkoa wa Liaoning, Kaskazini Mashariki mwa China, Oktoba 18, 2023 . Ukifanyika chini ya kaulimbiu ya "Kuhimiza kwa nguvu Viwanda Vipya na Kujenga Uzalishaji Mpya", mkutano huo unalenga kukuza maendeleo ya utengenezaji wa bidhaa viwandani ambayo yanatumia teknolojia za akili bandia, njia bila kuchafua mazingira, na yaliyounganishwa. Mkutano huo umeandaa eneo la maonyesho ya mafanikio ya ubunifu lenye ukubwa wa mita za mraba 20,000, linalojikita katika mafanikio mapya zaidi katika maendeleo ya viwanda vinavyotumia mtandao wa intaneti. (Xinhua/Chenwei)

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha