China yajiandaa kurusha kwenye anga ya juu chombo cha Shenzhou-17

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 20, 2023
China yajiandaa kurusha kwenye anga ya juu chombo cha Shenzhou-17
Picha hii iliyopigwa Oktoba 19, 2023 ikionyesha muunganiko wa chombo cha kubeba wanaanga kwenye anga ya juu cha Shenzhou-17 na roketi ya kubeba ya Long March-2F kwa pamoja vikiandaliwa tayari kuhamishwa hadi eneo la kurusha vyombo vya anga ya juu la Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Jiuquan, Kaskazini-Magharibi mwa China. (Picha na Wang Jiangbo/Xinhua)

JIUQUAN – Muunganiko wa chombo cha kubeba wanaanga kwenye anga ya juu cha Shenzhou-17 na roketi ya kubeba ya Long March-2F kwa pamoja vimehamishwa hadi eneo la kurusha vyombo vya anga ya juu siku ya Alhamisi, Shirika la Anga ya Juu la China (CMSA) limesema.

Kwa mujibu wa CMSA, nyenzo na vifaa kwenye eneo la urushaji vyombo vya anga ya juu viko katika hali nzuri, na ukaguzi wa ufanisi wa kabla ya urushaji wa chombo na majaribio ya pamoja yatafanywa kama ilivyopangwa. Chombo hicho kitarushwa kwenye anga ya juu kwa wakati unaofaa katika siku za usoni.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha