Katika picha: mashamba ya chumvi katika Mkoa wa Tibet nchini China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 23, 2023
Katika picha: mashamba ya chumvi katika Mkoa wa Tibet nchini China
Wanakijiji wakifanya kazi kwenye shamba la chumvi lililoko Wilaya ya Kabila la Wanaxi wa kaunti ya Markam katika Mji wa Qamdo, Mkoa unaojiendesha wa Tibet, Kusini-Magharibi mwa China, Oktoba 20, 2023.(Xinhua/Sun Fei)

Kaunti ya Markam ulioko Mji wa Qamdo katika Mkoa unaojiendesha wa Tibet, Kusini-Magharibi mwa China unajulikana kwa kuwa mahali penye rasilimali nyingi za chumvi tangu China ya kale. Mashamba ya chumvi hujengwa hasa kwenye miteremko ya miamba na kando za Mto Lancang. Wenyeji wa mji huo ambao ni watu wa Kabila la Wanaxi hutengeneza mvuke kwa kukausha maji chumvi kwenye jua kwa kutumia mbinu za mababu tangu Enzi ya Tang (618-907 AD).

Kwa kuwa na kiasi kikubwa cha pato la kila mwaka la bidhaa za chumvi, uzalishaji wa chumvi umekuwa chanzo kikuu cha mapato kwa watu wenyeji. Zaidi ya hayo, mashamba ya chumvi na desturi za kitamaduni katika eneo hili huwa kivutio cha kipekee kwa watalii.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha