

Lugha Nyingine
Mkutano wa Kutangaza Maonyesho ya Nyaya za Seng’enge ya Anping China Mwaka 2023 wafanyika Beijing (3)
Ukiwa na kaulimbiu ya "Anping Nyekundu, Mji Mashuhuri wa kutengeneza Nyaya za Seng’enge Duniani", Mkutano wa Beijing wa Kutangaza Maonyesho ya Kimataifa ya Nyaya za Seng’enge ya Anping China Mwaka 2023 yanayoandaliwa na Kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ya Anping na Serikali ya Anping umefanyika katika Studio Namba 1 ya Gazeti la People's Daily hapa Beijing, China.
Mkutano huo umepata usaidizi mkubwa kutoka Chuo cha Sayansi cha Hebei, Idara ya Viwanda na Teknolojia ya Habari ya Mkoa wa Hebei, na Idara ya Biashara ya Mkoa wa Hebei.
Katika hotuba yake kwenye mkutano huo, Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Kamati ya mji wa Hengshui wa CPC na Mkurugenzi wa Idara ya Uenezi ya Hengshui Liu Libin amesema kuwa, baada ya kufanyika kwa miaka 22, maonyesho hayo yamekuwa shughuli muhimu ya kukuza utamaduni wa sekta ya nyaya za Seng’enge, kuonyesha bidhaa za teknolojia ya hali ya juu, na kupanua ushirikiano na mabadilishano.
Amesema kuwa yamekuwa ni jukwaa la kimataifa na limekadiriwa kuwa sehemu ya maonyesho bora ya Mkoa wa Hebei. Pia ni jukwaa muhimu kwa Hengshui kufungua mlango, kufanya mabadilishano na ushirikiano, na kuongeza uwekezaji wa kiuchumi na biashara.
“Maonyesho ya Kimataifa ya Nyaya za Seng’enge ya Anping China Mwaka 2023 yatafanyika katika Kituo cha Maonyesho cha Kimataifa cha Anping kuanzia Oktoba 22 hadi 24." Cao Xiangdong, Katibu wa Kamati ya Anping ya CPC amesema katika hotuba yake kwenye mkutano huo.
Amesema shughuli mbalimbali za kibiashara kama vile mikutano ya moja kwa moja ya manunuzi kwa wanunuzi wa kitaalamu kutoka nje na uonyeshaji wa mafanikio ya kisayansi na kiteknolojia utafanyika wakati wa maonyesho hayo. Amesema, maonyesho hayo yamepata mafanikio mapya katika ukubwa wa maonyesho, idadi ya wafanyabiashara wa kigeni, na ushawishi wa maonyesho.
Imefahamika kuwa, vibanda 420 vya aina mbalimbali vimejengwa katika maonyesho haya, idadi ambayo imeongezeka maradufu ikilinganishwa na mwaka jana. Miongoni mwa waonyeshaji bidhaa wanaoshiriki katika maonyesho hayo, zaidi ya 56% wanatoka nje ya Anping, na zaidi ya 80% ya waonyeshaji wa mashine wanatoka nje ya Anping. Aidha, ushiriki wa wafanyabiashara wa kigeni umeongezeka kwa kiasi kikubwa, huku wafanyabiashara 138 kutoka Russia, Singapore, Saudi Arabia na nchi nyingine wamethibitisha kushiriki katika maonyesho hayo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma