Nguzo kuu ya daraja lenye urefu wa kwenda juu zaidi duniani yakamilika kujengwa Kusini Magharibi mwa China (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 25, 2023
Nguzo kuu ya daraja lenye urefu wa kwenda juu zaidi duniani yakamilika kujengwa Kusini Magharibi mwa China
Wafanyakazi wakifanya kazi kwenye nguzo kuu ya daraja la genge kuu la Huajiang katika Mkoa wa Guizhou, Kusini-Magharibi mwa China, Oktoba 24, 2023. (Xinhua/Tao Liang)

GUIYANG – Ujenzi wa nguzo kuu ya mwisho ya daraja la genge kuu la Huajiang umekamilika siku ya Jumanne katika Mkoa wa Guizhou, Kusini Magharibi mwa China, na kuashiria hatua kubwa katika ujenzi wa daraja hilo lenye urefu wa kwenda juu zaidi duniani.

Likiwa limesanifiwa kuwa na urefu wa mita 625 kati ya sitaha ya daraja na chini ya Mto Beipanjiang, daraja hilo la Huajiang litakuwa lenye urefu wa kwenda juu zaidi duniani baada ya kukamilika Mwaka 2025.

Daraja hilo lenye urefu wa mita 2,890 linapatikana katika Kaunti inayojiendesha ya Makabila ya Wabouyei na Wamiao ya Guanling na ni sehemu ya barabara kuu inayounganisha eneo maalum la Liuzhi ya Mji wa Liupanshui na Kaunti ya Anlong ya Eneo linalojiendesha la Makabila ya Wabouyei na Wamiao la Qianxinan katika Mkoa wa Guizhou.

Wang Chaoguo, meneja wa mradi huo, amesema imechukua siku zaidi ya 670 kuendelea kutoka katika ujenzi wa msingi wa zege hadi kukamilika kwa nguzo hiyo kuu, na timu ya wajenzi itaendelea kufanyia kazi muundo wa daraja hilo.

Daraja hilo litapunguza muda wa kuvuka genge hilo kutoka dakika 70 hadi takriban dakika moja, jambo ambalo litasaidia kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya wenyeji, pamoja na ustawi wa vijijini.

Ukiwa unapatikana kati ya milima na magenge, Mkoa wa Guizhou ni nyumbani kwa karibu nusu ya madaraja 100 yenye urefu wa kwenda juu zaidi duniani.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha