Mwakilishi wa Louisiana kupitia chama cha Republican Mike Johnson achaguliwa spika mpya wa bunge la Marekani baada ya wiki kadhaa za mivutano (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 26, 2023
Mwakilishi wa Louisiana kupitia chama cha Republican Mike Johnson achaguliwa spika mpya wa bunge la Marekani baada ya wiki kadhaa za mivutano
Mandhari ya Ukumbi wa Bunge la Marekani wakati wa kuita majina kwenye upigaji kura wa kumchagua spika mjini Washington, D.C., Marekani, Oktoba 25, 2023. (Picha na Aaron Schwartz/Xinhua)

WASHINGTON - Mwakilishi wa Louisiana kupitia chama cha Republican, Mike Johnson, ambaye ni makamu mwenyekiti wa Kambi ya Wabunge wa Chama cha Republican katika Bunge la Marekani, amechaguliwa kuwa spika mpya wa bunge kwenye upigaji kura uliofanyika Jumatano, na kufanya mivutano ya wiki kadhaa kukoma kwa muda wakati Wabunge wa Chama cha Republican walipokuwa wakihangaika kutafuta mbadala wa spika kufuatia kuondolewa madarakani kulikoweka kihistoria kwa Spika Kevin McCarthy.

Johnson, mgombea wa nne wa chama cha Republican, ameshinda kwa kupata kura 220 za Ndiyo na 209 na Hapana, huku akipata uungwaji mkono wa wabunge wote wa chama cha Republican.

Wagombea waliopitishwa hapo awali -- Kiongozi wa Wabunge walio Wengi Bungeni Steve Scalise, Mbunge nambari 2 wa Republican katika Baraza la Wawakilishi, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria Jim Jordan, na Kiongozi wa Shughuli Bungeni za Wabunge Walio Wengi Tom Emmer -- wote walishindwa kupata kura za kutosha za Republican zinazohitajika kuvuka idadi inayotakiwa.

Siku ya Jumanne, McCarthy alisema chama chake kilikuwa "mahali pabaya sana" huku baadhi ya wabunge wakiendelea kushikilia msimamo wao dhidi ya kumuunga mkono aliyeteuliwa kuwa spika.

Johnson, anayechukuliwa kuwa mhafidhina katika chama cha Republican, amefanikiwa kupata kura kutoka kwa wahafidhina wa mrengo wa kulia ambao walimkosoa McCarthy, na kutoka kwa watu wa mrengo wa wastani ambao walimpinga Jordan mwenye msimamo mkali.

Bunge hilo limekuwa halina kiongozi kwa wiki tatu, baada ya McCarthy kuondolewa katika nafasi yake Oktoba 3, kwa hoja iliyoanzishwa na mwanachama mhafidhina wa chama chake. Warepublican wanane walipiga kura kuungana na wabunge wa Chama cha Democrats katika kuondolewa kwake kulikoweka rekodi ya kihistoria.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha