Huawei yazindua mpango wa kutoa mafunzo ya Teknolojia ya Habari nchini Zimbabwe (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 26, 2023
Huawei yazindua mpango wa kutoa mafunzo ya Teknolojia ya Habari nchini Zimbabwe
Picha hii iliyopigwa Oktoba 24, 2023 inaonyesha wapokea mafunzo wa programu ya Seeds for the Future kwa Mwaka 2023 wakiwa kwenye uzinduzi wa programu hiyo mjini Harare, Zimbabwe, Oktoba 24, 2023. (Xinhua/Tafara Mugwara)

HARARE - Kampuni kubwa ya mawasiliano ya China Huawei imezindua rasmi programu ya Seeds for the Future kwa Mwaka 2023 nchini Zimbabwe, yenye lengo la kukuza vipaji vya wenyeji katika sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Jumla ya wanafunzi 50 wa shahada ya kwanza kutoka vyuo vikuu vya Zimbabwe watapitia mafunzo ya mtandaoni ya wiki moja ili kuboresha maarifa na ujuzi wao wa TEHAMA kuanzia Novemba 20 hadi 27.

Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Naibu Waziri wa Elimu ya Juu na Ufundi Simelisizwe Sibanda, Mke wa Rais wa Zimbabwe na Mlezi wa Programu ya Seeds for the Future, Auxillia Mnangagwa, amesema kuwajengea vijana ujuzi wa TEHAMA ni jambo la lazima kwani dunia inapitia mapinduzi ya teknolojia ya kidijitali.

Wakati Zimbabwe inajitahidi kuendeleza sekta yake ya TEHAMA kwa ajili ya mageuzi ya kiuchumi, kuna pengo kati ya maarifa yanayofundishwa darasani na ujuzi ambao ni muhimu katika ulimwengu wa kisasa, amesema Mnangagwa.

"Kupitia programu ya Seeds for the Future na jitihada nyingine, Huawei inasaidia kushughulikia tatizo hili," amebainisha, huku akiishukuru Huawei kwa msaada wake katika uhamishaji wa ujuzi na maendeleo ya miundombinu.

Yang Shengwan, Mkurugenzi Mkuu wa Huawei nchini Zimbabwe, amesema Huawei inaendesha shindano la Seeds for the Future, Akademia ya TEHAMA, Mashindano ya TEHAMA, mafunzo ya kivitendo kazini, programu za kuajiri katika vyuo vikuu ili kuendeleza teknolojia za TEHAMA na vipaji vya TEHAMA nchini Zimbabwe.

Amesema tangu programu hiyo ilipoanzishwa kwa mara ya kwanza nchini Zimbabwe Mwaka 2015, wizara husika na vyuo vikuu vya nchini humo vimefanya kazi pamoja ili kutoa fursa ya kujifunza kuhusu teknolojia ya kisasa ya TEHAMA na wanafunzi wapatao 1,245 wamepatiwa mafunzo katika Akademia ya TEHAMA ya Huawei.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha