Wanaanga wa China wa Chombo cha Shenzhou-17 waingia kwenye kituo cha anga ya juu, kukamilisha makabidhiano ndani ya siku nne (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 27, 2023
Wanaanga wa China wa Chombo cha Shenzhou-17 waingia kwenye kituo cha anga ya juu, kukamilisha makabidhiano ndani ya siku nne
Picha hii iliyopigwa katika Kituo cha Udhibiti wa Safari ya Anga ya Juu cha Beijing Oktoba 26, 2023 ikionyesha Wanaanga wa China wa Chombo cha Shenzhou-16 na Shenzhou-17 wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya kituo cha anga ya juu cha China. (Picha na Han Qiyang/Xinhua)

Beijing - Wanaanga watatu wa China waliosafiri na chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-17 wameingia kwenye kituo cha anga ya juu cha China na kukutana na wanaanga wengine watatu siku ya Alhamisi, wakianza raundi mpya ya makabidhiano ya wanaanga kwenye obiti ya anga ya juu.

Wanaanga wa Chombo cha Shenzhou-16 walifungua mlango wa kituo hicho saa 1:34 jioni. (Kwa saa za Beijing). Wanaanga hao ambao wako kwenye kituo hicho cha anga ya juu waliwasalimu wanaanga hao wapya, na wakapiga picha za pamoja.

Tang Hongbo, Kamanda wa kamisheni ya safari ya Chombo cha Shenzhou-17, alishuhudia wakati huo wa kihistoria akiwa ni mmoja wa wanaanga wa kundi la kwanza wa China kwenye kituo cha anga ya juu cha China Mwezi Juni, 2021 alipoingia kwenye obiti kwa Chombo cha Shenzhou-12.

Sasa, mapitio ya anga ya juu ya Tang yamepanuliwa hadi kwenye maabara ya angani yenye moduli mbili za ziada na vifaa vya kisasa zaidi vya majaribio. Pia ameweka rekodi mpya ya muda mfupi zaidi kati ya safari mbili za anga ya juu kwa wanaanga wa China.

Kukusanyika pamoja kwenye anga ya juu kwa wanaanga hao wa vyombo viwili tofauti kumeanzisha raundi ya tatu ya kubadilisha zamu ya wanaanga katika obiti kwenye kituo cha anga ya juu cha China.

Kwa mujibu wa Shirika la Anga ya Juu la China, wanaanga hao sita wataishi na kufanya kazi pamoja kwa takriban siku nne kukamilisha kazi zilizopangwa na kazi ya makabidhiano.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha