

Lugha Nyingine
Maua yaliyozalishwa kwenye anga ya juu yachanua katika Mkoa wa Yunnan, Kusini-Magharibi mwa China
KUNMING - Mnamo Agosti 2022, mbegu zaidi ya 8,000 za maua ziliwasili katika kituo cha uhandisi cha utafiti wa maua cha Kampuni ya Yunnan Jinke katika Mji wa Anning, Mkoa wa Yunnan, Kusini-Magharibi mwa China baada ya kusafirishwa kwenye anga ya juu kwa kupanda chombo cha Shenzhou.
Uzalishaji mbegu za maua kwenye anga ya juu huhusiana hasa na kuziweka mbegu au sehemu za mimea kwenye mionzi ya ulimwengu na nguvu ya mvutano ya anga ya juu ili kubadilisha jeni zao, kwa ajili ya kuunda spishi mpya au aina nyingine zenye ufanisi mkubwa kama vile vipindi vifupi vya ukuaji, mavuno mengi na uhimilivu bora kwa magonjwa.
Kwa mujibu wa Tian Liantong, mwanateknolojia wa kituo cha uhandisi cha utafiti wa maua cha Kampuni ya Yunnan Jinke, kwa kawaida huchukua miaka mitano kuzalisha aina mpya za maua ambazo watumiaji wanaweza kununua sokoni, na baadhi ya spishi huhitaji miaka kumi kupitia mchakato huo kutoka hatua ya kuzaliana hadi kuwa bidhaa, kwani zinapaswa kupitia hali mbalimbali na ngumu za ukuaji ikiwa ni pamoja na halijoto, unyevunyevu na usambazaji wa lishe.
Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya mitaa ya Yunnan na taasisi za utafiti wa kisayansi pamoja na kampuni za biashara zimekuwa zikifanya juhudi kubwa katika kuotesha mbegu kwenye anga ya juu, na kuzalisha aina mpya za maua ili kuongeza usambazaji wa maua sokoni. Hadi kufikia mwisho wa Mwaka 2022, spishi mya za maua zaidi ya 950 zimekuzwa kwa kujitegemea ndani ya Mkoa wa Yunnan na spishi zaidi ya 1,000 za maua zilizoanzishwa zimerekodiwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma