

Lugha Nyingine
Wanakijiji wakikausha mazao kwa jua huko Wuyuan, Mkoa wa Jiangxi, Mashariki mwa China (6)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 30, 2023
![]() |
Mkulima akipanga mazao yake ili kuyakausha kwa jua katika Kijiji cha Huangling cha Wilaya ya Wuyuan katika Mji wa Shangrao, Mkoa wa Jiangxi, Mashariki mwa China. (People's Daily Online/Zhu Haipeng) |
Kijiji cha Huangling cha Wilaya ya Wuyuan katika Mji wa Shangrao, Mkoa wa Jiangxi, Mashariki mwa China kimebadilika kama picha ya kuchorwa ya rangi mbalimbali ya mavuno ya mazao mengi ya kilimo huku wanakijiji wakikausha kwa jua mazao mbalimbali ya kilimo, hali ambayo inavutia watalii wengi.
Kuanzia wakati wa zaidi ya miaka 580 iliyopita, kijiji hicho kinafurahia mandhari nzuri ya mazingira ya asili, ambapo kuna majengo zaidi ya 100 ya kale ya mtindo wenye sifa za Kabila la Wahui wa rangi nyeupe na kijivu.
Katika tangazo la hivi punde la Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UNWTO), kijiji hicho kimepata nafasi ya kutamanika kwenye orodha ya "Vijiji Bora vya Utalii" kwa Mwaka 2023.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma