Safari ya kuvutia kwenye Jumba la Makumbusho ya Jiolojia la Guizhou: Mawasiliano kati ya zama za kale na sasa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 02, 2023
Safari ya kuvutia kwenye Jumba la Makumbusho ya Jiolojia la Guizhou: Mawasiliano kati ya zama za kale na sasa
Ukumbi unaoonesha katuni hai za viumbe vya kale ukutani kwa mfumo wa 3D kwenye Jumba la Makumbusho ya Jiolojia la Mkoa wa Guizhou, China. (Picha na Yang Qian/People’s Daily Online)

Ujumbe wa wanahabari wa vyombo vya habari kutoka nchi za Eurasia wa “Kuitazama Guizhou kupitia Vyombo vya Habari” Jumatatu ya Oktoba 27 walitembelea Jumba la Makumbusho ya Jiolojia la Mkoa wa Guizhou, China, ili kufahamu historia ya mkoa huo kubadilika kutoka bahari hadi eneo la milima. “Sampuli za madini zinazooneshwa kwenye jumba la makumbusho ya jiolojia la Guizhou kwakweli ni zenye kunifungua macho” amesema Umatkul Bralkieva, meneja wa mambo ya kibiashara wa gazeti la Slovo Kyrgyzstana la Kyrgyzstan.

Jumba la Makumbusho ya Jiolojia la Mkoa wa Guizhou lipo kwenye eneo la Ziwa Guanshan huko Guiyang, mji mkuu wa Mkoa wa Guizhou, China. Jumba hilo lina eneo la majengo lenye ukubwa wa mita za mraba 40,000 na eneo la maonesho lenye ukubwa wa mita za mraba 15,000. Ni jumba la makumbusho ya sayansi asilia linalomilikiwa na serikali lenye eneo kubwa zaidi la majengo mkoani Guizhou.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha