Picha: Bidhaa zenye rangi ya kuvutia macho kwenye Maonyesho ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 06, 2023
Picha: Bidhaa zenye rangi ya kuvutia macho kwenye Maonyesho ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE)
Picha ikionesha panda Jin Bao, maskoti wa Maonesho ya CIIE inayoundwa kwa matofali ya kuchezea akionyeshwa kwenye eneo la mabanda ya bidhaa la maonyesho hayo, tarehe 5, Novemba. (Picha na Li Meiyu/People’s Daily Online Swahili)

Maonyesho ya sita ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) yameanza jana Jumapili mjini Shanghai na yamepangwa kuendelea kufanyika hadi tarehe 10, Novemba. Kuanzia maskoti rasmi wa maonyesho hayo, panda Jin Bao, matunda ya joka ya njano kutoka Ecuador na kazi za sanaa zenye umbo la kipepeo ambazo ni rafiki kwa mazingira……bidhaa zenye rangi za kuvutia zilizoletwa na kampuni washiriki zimevutia macho ya watembeleaji wengi wa maonyesho.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha