Reli ya mwendokasi ya Jakarta-Bandung yakaribishwa na abiria nchini Indonesia (7)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 06, 2023
Reli ya mwendokasi ya Jakarta-Bandung yakaribishwa na abiria nchini Indonesia
Abiria wakisubiri kwenye foleni ili kupanda treni ya kwanza ya mwendokasi ya Reli ya Jakarta-Bandung katika Stesheni ya Reli ya Halim mjini Jakarta, Indonesia, Novemba 5, 2023. (Xinhua/Xu Qin)

Reli ya Mwendokasi ya Jakarta-Bandung (HSR), inayounganisha Mji wa Jakarta na Mji wa Bandung ambao ni mji wa nne kwa ukubwa nchini Indonesia, ni mradi kinara unaounganisha Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) la China na mkakati wa Indonesia wa Egemeo la Baharini la Dunia.

Kuanzia Oktoba 17 hadi Oktoba 31, idadi kubwa ya abiria wa kila siku kwenye reli hiyo ilizidi 14,200. Tiketi zaidi ya 165,000 ziliuzwa kuanzia Oktoba 17 hadi Novemba 4. Reli hiyo imeongeza ratiba yake hadi usafiri wa treni 28 kwa siku, kutoka usafiri wa treni 14 za awali, kuanzia Novemba 1.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha