

Lugha Nyingine
“Janga katika Ukanda wa Gaza linahitaji usimamishaji wa mapigano wa haraka wa kibinadamu”
![]() |
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Novemba 6, 2023. (Xinhua/Xie E) |
UMOJA WA MATAIFA - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kwamba maafa yanayotokea Gaza yanafanya usimamishaji wa mapigano wa kibinadamu kuwa wa dharura zaidi kila saa inayopita.
Jinamizi la Gaza ni zaidi ya janga la kibinadamu. Ni mgogoro wa ubinadamu. Mgogoro huo unaozidi kutikisa Dunia, kuleta hali isiyo ya tulivu katika kanda hiyo, cha kusikitisha zaidi ni kwamba unaharibu maisha ya watu wengi wasio na hatia, amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatatu.
Operesheni za ardhini za Jeshi la Israel na mashambulizi ya makombora yanayoendelea yanawashambulia raia, hospitali, kambi za wakimbizi, misikiti, makanisa na vituo vya Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na makazi. Hakuna aliye salama. Wakati huo huo, Kundi la Hamas na wanamgambo wengine hutumia raia kama ngao za binadamu na wanaendelea kurusha makombora kiholela kuelekea Israel, amesema.
Gaza inakuwa kaburi la watoto. Mamia ya wasichana na wavulana wanaripotiwa kuuawa au kujeruhiwa kila siku. Waandishi wa habari wengi zaidi wameripotiwa kuuawa katika kipindi cha wiki nne zilizopita kuliko katika mgogoro wowote uliotokea miongo mitatu iliyopita. Wafanyakazi zaidi wa Umoja wa Mataifa wameuawa kuliko katika kipindi chochote cha kulinganishwa katika historia ya umoja huo, amesema.
"Janga linaloendelea linaufanya usimamishaji wa mapigano wa kibinadamu uwe wa haraka zaidi kila saa inayopita. Pande husika za mgogoro huo - na, kwa hakika, jumuiya ya kimataifa - zinakabiliwa na jukumu la haraka na la msingi: kukomesha mateso ya pamoja yasiyo ya kibinadamu na kupanua kwa kasi misaada ya kibinadamu kwa Gaza," Guterres amesema.
Amesema kuwa, Umoja wa Mataifa na washirika wake wametangaza ombi la msaaada wa kibinadamu wenye thamani ya dola bilioni 1.2 za Marekani kusaidia watu milioni 2.7 - wakazi wote wa Gaza na Wapalestina nusu milioni katika Ukingo wa Magharibi, ikiwa ni pamoja na Jerusalem Mashariki.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma