

Lugha Nyingine
Wanajeshi wa Israel wafikia "kiini cha mji wa Gaza" baada ya mwezi mmoja wa vita (3)
![]() |
Picha hii iliyotolewa na Jeshi la Ulinzi la Israel Novemba 7, 2023 ikionyesha wanajeshi wa Israel wakiendelea na operesheni za ardhini katika Ukanda wa Gaza. (Xinhua) |
JERUSALEM - Wanajeshi wa Israel walikuwa wakipigana siku ya Jumanne kwenye “kiini cha Mji wa Gaza” huku wanajeshi wa ardhini wa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) wakiendelea kusonga mbele katika Ukanda wa Gaza, hadi katikati mwa Mji wa Gaza, kamanda mwandamizi wa Jeshi la Israel amesema katika siku ya 32 ya mapambano kati ya Israel na Kundi la Hamas ambayo yamesababisha vifo zaidi ya Wapalestina 10,328 katika Ukanda wa Gaza.
Kwenye mahojiano na Shirika la Habari la ABC, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema, kuna uwezekano wa "kusimamisha vita kidogo kimbinu" katika mapigano ili kuruhusu misaada kufika Gaza au kuwezesha kuachiliwa huru kwa mateka karibu 240 waliotekwa nyara na Kundi la Hamas wakati wa mashambulizi yake ya Oktoba 7 dhidi ya Israeli.
Hata hivyo, Netanyahu amekataa makubaliano yoyote ya kusimamisha vita isipokuwa pale mateka wote watakapoachiliwa.
Baada ya vita kumalizika Gaza, Israel itachukua "jukumu la usalama la pande zote" katika Ukanda wa Gaza "kwa muda usiojulikana," Netanyahu amesema.
"Askari wetu wanaua magaidi, wanagundua mahandaki, wanaharibu silaha na wanaendelea kusonga mbele hadi katikati ya adui," Afisa Mkuu wa Kamandi ya Kusini ya Jeshi la Israel, Yaron Finkelman amesema katika taarifa kwa vyombo vya habari.
Waisraeli walikaa kimya kwa muda nchini kote kuwaomboleza watu wanaofariki kwenye mashambulizi ya Hamas siku ya Jumanne Oktoba 7.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma