Kivuko cha Khunjerab, bandari kuu ya nchi kavu inayounganisha China na Pakistan

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 08, 2023
Kivuko cha Khunjerab, bandari kuu ya nchi kavu inayounganisha China na Pakistan
Wasafiri wanaoelekea ng'ambo wakipanda basi la abiria kwenye Kivuko cha Khunjerab katika Eneo linalojiendesha la Kabila la Watajik la Taxkorgan, Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang, Kaskazini-Magharibi mwa China, Novemba 6, 2023. (Xinhua/Ding Lei)

Kikiwa kinapatikana katika Eneo linalojiendesha la Kabila la Watajik la Taxkorgan, Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang, Kaskazini-Magharibi mwa China, Kivuko cha Khunjerab ni bandari kuu ya nchi kavu kwenye mpaka wa China na Pakistani, kituo kikuu cha biashara kati ya China na Pakistani, na lango muhimu la kuingia Asia Kusini na Ulaya.

Tangu kuanza upya kwa utoaji vibali vya forodha kwa abiria Mwezi Aprili 3, 2023, Kivuko cha Khunjerab kimerekodi abiria zaidi ya 40,000 wanaoingia na kutoka.

Wakati wa Mkutano wa Tatu wa Baraza la Ushirikiano wa Kimataifa wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, China na Pakistan zilitoa taarifa za pamoja kwa vyombo vya habari na kutangaza kuwa Kivuko cha Khunjerab kitafanya kazi mwaka mzima, jambo ambalo litatoa mchango muhimu katika kuhimiza mabadilishano ya kiuchumi na kitamaduni kati ya China na Pakistani. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha