Katika picha: Teknolojia za hali ya juu zinazoonyeshwa kwenye Maonyesho ya 6 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 10, 2023
Katika picha: Teknolojia za hali ya juu zinazoonyeshwa kwenye Maonyesho ya 6 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE)
Watembeleaji wa maonyesho wakitazama muundo wa mfano wa gari linalojiendesha lenyewe banda la Kampuni ya magari ya Hyundai Mobis katika Maonyesho ya 6 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) mjini Shanghai, Mashariki mwa China, Novemba 9, 2023. (Xinhua/Xin Mengchen)

Kuanzia roboti mbalimbali zinazotumia teknolojia za akili bandia kama vile roboti mbwa, magari yanayojiendesha yenyewe, uvumbuzi wa upandaji mimea ya kilimo hadi mifumo ya vifaa tiba vya kisasa, teknolojia za hali ya juu zimewavutia watembeleaji wengi kwenye mabanda mbalimbali ya Maonyesho ya 6 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) yaliyofanyika Shanghai, Mashariki mwa China, Novemba 5 na yamepangwa kukamilika leo Ijumaa, Novemba 10.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha