Kampuni za China zatamani kupanua mitandao ya biashara kwenye maonyesho ya TransMEA (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 10, 2023
Kampuni za China zatamani kupanua mitandao ya biashara kwenye maonyesho ya TransMEA
Modeli ya treni ya mwendokasi ya China ikionyeshwa kwenye Maonyesho ya Teknolojiza za Kisasa za Usafiri, Ugavi, Miundombinu na usimamizi wa usafirishaji kwa nchi za Mashariki ya Kati na Afrika huko Cairo, Misri, Novemba 7, 2023. (Xinhua/Ahmed Gomaa)

CAIRO - Maonyesho ya 5 ya Kimataifa ya Teknolojiza za Kisasa za Usafiri, Ugavi, Miundombinu na usimamizi wa usafirishaji ya Mashariki ya Kati na Afrika TransMEA yamevutia kampuni za China, ambazo zina shauku ya kushiriki kwenye maendeleo ya usafiri katika eneo la Mashariki ya Kati, hasa nchini Misri.

Maonyesho hayo yaliyofanyika New Cairo kuanzia Novemba 5 hadi 8 kwa ufadhili wa Wizara ya Uchukuzi ya Misri yamevutia kampuni karibu 350 kutoka nchi 20 kuonesha teknolojia, suluhisho na bidhaa zao, zinazohusiana na nyanja za reli, treni ya chini ya ardhi, reli moja, usafiri wa vyombo vinavyotumia umeme, barabara na madaraja, usalama wa usafirishaji, usafiri wa baharini, bandari na ugavi, pamoja na teknolojia za habari na mawasiliano.

Meng Xiaohong, Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Mawimbi na Mawasiliano ya Reli ya China, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwamba kampuni yake inathamini maonyesho hayo kama fursa ya kutangaza bidhaa na utambuzi wa chapa nchini Misri na Mashariki ya Kati kwa ujumla.

Kampuni ya Mashine nzito ya Qingdao Haixi kutoka China pia imetamani uwezo wa maonyesho hayo kuhusu ujenzi wa kituo cha bandari.

Meng Wei, mkurugenzi wa biashara ya kimataifa wa kampuni hiyo, amesema katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, kampuni hiyo ilipewa kandarasi za kujenga mitambo ya kubeba kontena katika Bandari ya Alexandria na Kituo cha Kontena cha Damietta Alliance S.A.E. nchini Misri na sasa inatarajia kutoa huduma zaidi.

Amr Ismail, mjumbe wa bodi ya Kampuni ya magari ya Geyushi ya Misri akishiriki maonyesho hayo na mshirika wake wa China, Kampuni ya Shandong Heavy Industry, amesema wateja wengi zaidi wa nchi za kiarabu sasa wanaamini katika ubora wa bidhaa za China.

"Kwa mabasi makubwa na malori ya kubeba vitu vizito, dhamana ni muhimu sana, na mshirika wetu wa China anaweza kushinda kampuni za Ulaya katika suala hili," amebainisha, huku akiongeza kuwa "kampuni za China zinatoa bidhaa na huduma bora kwa bei nafuu."

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha