Mandhari ya Usiku ya Gurudumu kubwa la kuzunguka angani la kutazama mandhari la Glory Bay katika Mji wa Shenzhen, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 14, 2023
Mandhari ya Usiku ya Gurudumu kubwa la kuzunguka angani la kutazama mandhari la Glory Bay katika Mji wa Shenzhen, China
Picha hii iliyopigwa Novemba 13, 2023 ikionyesha watu wakifurahia mandhari ya usiku ya gurudumu kubwa la kuzunguka angani la kutazama mandhari la Glory Bay lililoko katika Bustani ya Utamaduni ya Binhai ya Eneo la Baoan la Mji wa Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, Kusini Mashariki mwa China. (Picha/People’s Daily Online)

Gurudumu kubwa la kuzunguka angani la kutazama mandhari na burudani "Glory Bay" lililoko katika Bustani ya Utamaduni ya Binhai ya Eneo la Baoan la Mji wa Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, Kusini Mashariki mwa China ni gurudumu kubwa zaidi katika Bara la Asia ambalo lilifunguliwa kwa umma Mwaka 2021, likiwa na urefu wa jumla wa mita 128 na vyombo (capsules) 28 vyenye uwezo wa kubeba watu 25 kila kimoja. Gurudumu hili ni alama mpya ya utamaduni wa mji wa Shenzhen iliyo ya kupendeza na kuupa shamrashamra mji huo ambao ni mji uliotangulia kutekeleza sera ya China ya mageuzi na kufungua mlango miaka 45 iliyopita na kuleta ustawi mkubwa wa kiuchumi si tu kwa China bali pia kwa nchi na maeneo yote duniani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha