Wilaya ya Bao'an katika Mji wa Shenzhen, China inavyounganisha ukale na usasa kuleta ustawi na uhifadhi wa ikolojia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 14, 2023
Wilaya ya Bao'an katika Mji wa Shenzhen, China inavyounganisha ukale na usasa kuleta ustawi na uhifadhi wa ikolojia
Waandishi wa habari wakipata maelezo kuhusu Masoko ya Kale ya Qingping yanayopatikana kwenye ukingo wa Mto Xinqiao katika eneo la Bao'an la Mji wa Shenzhen nchini China. (Picha/People’s Daily Online)

Masoko ya Kale ya Qingping yanapatikana kwenye ukingo wa Mto Xinqiao katika Kijiji cha Qiaotou kilichoko eneo la Bao'an la Mji wa Shenzhen nchini China. Yamejengwa kwa kuendana na daraja na yamepata ustawi wake kando ya mto. Mnamo Mwaka 1662, kwa kutegemea Mto Xinqiao, Daraja la Yongxing (daraja kuu la kale zaidi na la pekee la makaravati matatu katika Mji wa Shenzhen) lilijengwa, na eneo hilo lilikuwa kiini cha mtandao wa usafirishaji wa majini na ardhini. Kuanzia Mwaka 1796 hadi 1890, hatua kwa hatua eneo hili lilikuwa mahali pa kukusanyika kwa wafanyabiashara kwenye mwalo wa ukingo wa mashariki wa Mto Pearl katika zama za kale. Hadi sasa masoko na eneo zima hilo bado linaendelea kushikilia utaratibu wa kijadi wa masoko, utamaduni wa kucheza ngoma ya simba na opera ya Kikantoni.

Masoko haya yamekuwa na historia ya zaidi ya miaka 200. Pia yameorodheshwa kuwa mojawapo ya masoko makubwa manne ya kale katika Mji wa Shenzhen na yana hadhi muhimu ya kisiasa, kiuchumi na kitamaduni.

Serikali ya mtaa imekuwa ikifanya jitihada za kuhifadhi na kuendeleza eneo hili kupitia njia shirikishi na wakazi wa sehemu husika kwa kudumisha umaalum wa kihistoria na kitamaduni wa masoko ya kale, ulinzi na utumiaji wa majengo wenye ufanisi, na kufufua masoko ya zamani katika hali ya kupatana kati ya binadamu na mazingira zinazounganisha ukale na usasa. Kwa ujumla imekuwa ikitumia njia za kujenga upya eneo la awali la majengo, na kwa ujumla kuongeza nguvu ya uhai ya mji wa Qingping wenye masoko ya kale.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha