Thamani ya biashara ya mazao ya kilimo kati ya China na Afrika yatazamiwa kuzidi Dola za Kimarekani bilioni 10 mwaka 2023

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 15, 2023
Thamani ya biashara ya mazao ya kilimo kati ya China na Afrika yatazamiwa kuzidi Dola za Kimarekani bilioni 10 mwaka 2023
Tarehe 14, Novemba, wageni walioshiriki kwenye mkutano wa Baraza la Ushirikiano wa Kilimo wa China na Afrika wakitembelea katika Kituo cha Uvumbuzi wa Teknolojia ya Kilimo kilichoko Kijiji cha Damao, Eneo la Jiyang la Mji wa Sanya wa Mkoa wa Hainan wa China.

Mwaka 2023, thamani ya biashara ya mazao ya kilimo kati ya China na Afrika inatazamiwa kuzidi Dola za Kimarekani bilioni 10, ikiongezeka maradufu kuliko ile ya mwaka 2013. Hali hiyo ilijulishwa na Waziri wa Kilimo na Vijiji wa China Tang Renjian tarehe 14 kwenye mkutano wa pili wa Baraza la Ushirikiano wa Kilimo wa China na Afrika uliofanyika huko Sanya, Mkoa wa Hainan wa China.

Kwenye mkutano wa baraza hilo, Tang alisema, katika miaka ya hivi karibuni, mazao ya kilimo yenye sifa bora za kipekee iliyoagiza China kutoka nchi za Afrika yaliongezeka kwa kasi na kwa kiasi kikubwa, na hata wakati wa maambukizi ya UVIKO-19 ongezeko hilo lilidumisha zaidi ya asilimia 10 kila mwaka kwa wastani. Hadi mwisho wa mwaka 2021, uwekezaji wa kampuni za China katika bara la Afrika unaohusu kilimo umefikia Yuan za Renminbi bilioni 12.8, na wastani wa ongezeko ulifikia kwa asilimia 11.4 kila mwaka.

Tang alisema, katika muongo uliopita, China imejenga vituo 24 vya vielelezo vya teknolojia za kilimo barani Afrika, na kutembeza ufundi na teknolojia za kilimo zinazofaa barani Afrika kama vile za upandaji wa miche zaidi ya mahindi kwenye kila kitalu, kujenga mabanda ya upandaji mboga na kadhalika, hizo zote zimesaidia wastani wa ongezeko la uzalishaji wa kilimo wa nchi za Afrika kufikia asilimia 30 hadi 60.

Mkutano wa pili wa Baraza la Ushirikiano wa Kilimo la China na Afrika uliandaliwa na Wizara ya Kilimo na Vijiji ya China na serikali ya Mkoa wa Hainan wa China, na umefanyika kuanzia tarehe 13 hadi 15 huko Sanya, Hainan. Mkutano wa Baraza hilo umewaalika maofisa wa idara husika za kilimo za nchi mbalimbali za Afrika, mabalozi wa Afrika nchini China, na wajumbe kutoka Umoja wa Afrika na Umoja wa Mapinduzi ya Kijani wa Afrika kushiriki.

Inafahamika kuwa ili kusaidia maendeleo ya kisasa ya kilimo ya Afrika, China itaweka mkazo katika kusaidia Afrika kuongeza uwezo wa uzalishaji wa nafaka, kutekeleza mpango wa ushirikiano wa uvumbuzi wa teknolojia za kilimo, na mradi wa vielelezo wa kuondoa umaskini na kuwanufaisha wakulima.

Wakati wa mkutano huo, wageni walioshiriki wametembelea kituo cha kilimo cha kisasa cha Mkoa wa Hainan.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha