Mji Mdogo wa Kale wa Gankeng wa Shenzhen, China: Vijiji vya kale vya Kabila la Wakejia vyenye maisha ya hali ya utulivu mjini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 16, 2023
Mji Mdogo wa Kale wa Gankeng wa Shenzhen, China: Vijiji vya kale vya Kabila la Wakejia vyenye maisha ya hali ya utulivu mjini
Mwandishi wa habari wa Ubelgiji Fanny akitembelea katika mji mdogo wa kale wa Gankeng. (Picha na Zhang Wenjie/People’s Daily Online)

Mji mdogo wa kale wa Gankeng ulioko eneo la Longang la Mji wa Shenzhen wa China ni moja kati ya vijiji vikubwa 10 vya kale vya Shenzhen. Mji mdogo huo ulikuwa maskani ya watu wa kabila la Wakejia, na kwa hivyo umekuwa na utamaduni wa kipekee wa watu wa kabila hilo. Tarehe 14, Novemba, waandishi wa habari kutoka Ujerumani, Ubelgiji, Brazil, Tanzania na nchi nyingine mbalimbali waliingia kwenye Gankeng na kuona utamaduni wa kabila la Wakejia huko.

Gankeng ulikuwa kama kona “iliyosahauliwa”. Ili kudumisha utamaduni wa kabila la Wakejia wanaoishi Shenzhen, hivi sasa mji mdogo wa kale wa Gankeng umejengwa upya kuwa “mji mdogo wa kwanza kwa uvumbuzi wa utamaduni nchini China” unaojumisha utamaduni, ikolojia, teknolojia na utalii. Mji huo wenye historia ya miaka 350 sasa umepata tena uhai wake.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha