Maonyesho ya 25 ya Teknolojia ya Hali ya Juu ya China yafunguliwa mjini Shenzhen

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 16, 2023
Maonyesho ya 25 ya Teknolojia ya Hali ya Juu ya China yafunguliwa mjini Shenzhen
Maonyesho ya 25 ya Kimataifa ya Teknolojia ya Hali ya Juu ya China Mwaka 2023

Maonyesho ya 25 ya Kimataifa ya Teknolojia ya Hali ya Juu ya China Mwaka 2023 yamefunguliwa mjini Shenzhen katika Mkoa wa Guangdong, Kusini Mashariki mwa China siku ya Jumatano, yakichukua eneo kubwa zaidi kuwahi kutokea.

Maonyesho hayo yatakayofanyika kwa siku tano kuanzia Novemba 15 hadi 19 yanashirikishwa na nchi na maeneo zaidi ya 105 na kampuni 4,925.

Yakichukua eneo lenye ukubwa wa mita za mraba zaidi ya 500,000, maonyesho hayo yamekuwa makubwa zaidi pamoja na nchi na maeneo mengi zaidi yanayoshiriki katika historia ya maonyesho hayo.

Maonyesho hayo ya mwaka huu yenye kaulimbiu isemayo “Kuchochea Uhai wa Uvumbuzi na Kuongeza Ubora wa Maendeleo", yanafuata muundo wa "Onyesho moja na kumbi mbili", yakiweka maeneo ya maonyesho kwenye Kituo cha Mikutano na Maonyesho cha Shenzhen katika Wilaya ya Futian na Kituo cha Kimataifa cha Mikutano na Maonyesho katika Wilaya ya Bao'an.

Kati ya maeneo hayo, eneo la maonyesho la Futian lina mabanda ya maonyesho kama vile Maonyesho ya Mafanikio ya Uvumbuzi wa Sayansi na Teknolojia ya China, Maonyesho ya Mafanikio ya Uvumbuzi wa Sayansi na Teknolojia ya Kimataifa, na Maonyesho ya Huduma ya Teknolojia ya Hali ya Juu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha