Rais Xi Jinping atoa wito kwa pande wanachama wa APEC kuendelea na uvumbuzi, uwazi na kuhimiza maendeleo ya kikanda

(CRI Online) Novemba 20, 2023
Rais Xi Jinping atoa wito kwa pande wanachama wa APEC kuendelea na uvumbuzi, uwazi na kuhimiza maendeleo ya kikanda
(Picha inatoka Shirika la Habari la China Xinhua.)

Rais Xi Jinping wa China ametoa wito kwa pande wanachama wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki (APEC) kutafuta maendeleo yanayotokana na uvumbuzi, yaliyo wazi, ya kijani, na ambayo ni jumuishi yanayoleta manufaa ya pande zote katika kuhimiza maendeleo ya kikanda.

Rais Xi ameyasema hayo kwenye hotuba aliyoitoa Ijumaa kwenye mkutano wa Viongozi wa APEC mjini San Francisco, Marekani.

Rais Xi amesema China itaendelea na nia yake ya kuleta maendeleo ya amani, na kuongeza kuwa lengo la msingi la maendeleo ni kuwawezesha watu wa China kuishi maisha mazuri, si kuchukua nafasi ya mtu yeyote. Amekumbusha kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya kutimia miaka 45 tangu China ianze mageuzi na ufunguaji mlango, na kwamba China itaendelea kufuata maendeleo yenye ubora wa hali ya juu na yenye uwazi, na kwamba maendeleo ya China yanaweza kusaidia kuchangia kuifanya dunia kuwa ya kisasa.

Rais Xi pia ametoa wito wa kufanyika kwa juhudi za pamoja kuhimiza ushirikiano wa Asia na Pasifiki ili kupata matokeo yenye manufaa zaidi na kujenga miaka mingine 30 ushirikiano wenye manufaa wa Asia na Pasifiki.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha