Shenzhen yaweka jitihada katika kujenga mji ulio rafiki kwa watoto kwa mazingira yenye umaalum

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 20, 2023
Shenzhen yaweka jitihada katika kujenga mji ulio rafiki kwa watoto kwa mazingira yenye umaalum
Picha hii ya angani iliyopigwa Novemba 17, 2023 ikionyesha watoto na walezi wao wakicheza kwenye bustani ya watoto karibu na Stesheni ya Reli ya Shenzhen Kaskazini huko Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China. (Xinhua/Mao Siqian)

Mji wa Shenzhen ulizindua miongozo ya kwanza kwa nchi ya China kwa ajili ya kujenga mji rafiki kwa watoto miaka minane iliyopita. Tangu wakati huo mji huo umekuwa ukianzisha mfululizo wa hatua zinazoongoza ujenzi kuelekea kutimiza lengo hili.

Takwimu zinaonyesha kuwa hadi kufikia Oktoba 2023, vituo 452 vinavyofaa watoto katika ngazi ya mji na bustani zaidi ya 1,260 zimeanzishwa ili kuboresha hatua kwa hatua maeneo maalum ya shughuli za watoto na vifaa vya elimu mjini Shenzhen. Wakati huo huo, mashirika 580 ya mijadala ya watoto, nyumba za watoto 761 katika maeneo tofauti ya makazi na shule za chekechea zaidi ya 1,270 pameanzishwa ili kuboresha maisha ya watoto na kuleta urahisi kwa watoto kusafiri.

Neno "rafiki kwa watoto" huko Shenzhen limehamishwa kwa mafanikio kutoka kuwa dhana tu hadi maafikiano ya mji mzima na hatua za pamoja. Shenzhen itaendelea kufanya majaribio na kujitahidi kufikia lengo lake la kujenga mji ulio rafiki kwa watoto wenye umaalum wake.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha