Mpishi wa Mikate ya kisanaa ya kijadi awa maarufu na kupata fursa za soko

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 20, 2023
Mpishi wa Mikate ya kisanaa ya kijadi awa maarufu na kupata fursa za soko
Tian Xiao (katikati) akibadilishana maoni na marafiki zake kuhusu Mianhua. (Picha na Li Xin/Xinhua)

Mkate wa “Mianhua" pia hujulikana kwa jina la “Huamo”, ambalo maana yake ni mkate wenye umbo la kisanaa. Chanzo cha Mianhua ni katika desturi ya kutumia mkate wenye maumbo ya wanyama badala ya ng’ombe na mbuzi halisi katika shughuli za matambiko ya kijadi. Una historia ya zaidi ya miaka elfu. Katika sehemu mbalimbali za kaskazini mwa China, kuna utamaduni wa kuwazawadia Mianhua wanafamilia na marafiki ambao unaashiria kuwatakia amani na baraka njema.

Tian Xiao, ni mpishi wa Mianhua kutoka Mji wa Weifang katika Mkoa wa Shandong, Kusini mwa China. Akihamasishwa na familia yake alijifunza ufundi wa upikaji Mianhua wakati wa utoto. Baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu mwaka 2013, Tian alifungua duka nyumbani kwao, akifanya uvumbuzi katika misingi ya kijadi, ili kuzalisha mikate ya Mianhua inayopendwa na vijana na watoto. Mikate yake hiyo imewahi kuonyeshwa kwenye maonyesho na kushinda tuzo mbalimbali katika Mkoa wa Shandong na sehemu nyingine nchini China.

Mwaka 2022, Tian alikuja Beijing na mikate yake. Tian hutegemea majukwaa ya mauzo na maonyesho ya mtandaoni ili kuonesha kazi zake za mikate, na wakati huohuo akianzisha chumba chake cha sanaa ya mikate na kufundisha madarasa ili kuhamasisha ujuzi huu wa kijadi wa upikaji mianhua kwa vijana.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha