Ndege wanaohama wakionekana katika maeneo oevu Mkoani Fujian, Kusini Mashariki mwa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 20, 2023
Ndege wanaohama wakionekana katika maeneo oevu Mkoani Fujian, Kusini Mashariki mwa China
Ndege aina ya spoonbills wenye uso mweusi wakionekana kwenye eneo oevu la mlango wa Mto Minjiang katika Mkoa wa Fujian, Kusini-Mashariki mwa China, Novemba 15, 2023. (Xinhua/Wei Peiquan)

Makundi ya ndege wanaohama yameweka vituo vya muda katika Miji ya Fuzhou, Quanzhou na maeneo mengine katika Mkoa wa Fujian, Kusini-Mashariki mwa China wakati wakisafiri kuelekea kusini mwa China ili kuvuka majira ya baridi. Miongoni mwao, kuna ndege adimu, kama vile ndege aina ya spoonbills wenye uso mweusi na ndege aina ya spoon-billed sandpipers ambao wako chini ya ulinzi wa kitaifa wa daraja la kwanza nchini China, ambao idadi yao inaendelea kuongezeka.

Katika miaka ya hivi karibuni, Mkoa wa Fujian umeanzisha mfululizo wa miradi ya kufufua ikolojia ili kuimarisha juhudi katika ulinzi wa ardhi oevu, usimamizi wa mito, kushughulikia takataka baharini na kurejesha misitu. Pamoja na mazingira ya ikolojia kuboreshwa siku hadi siku, Mkoa wa Fujian unavutia idadi kubwa ya ndege wanaohama kuja hapa kwa majira ya baridi na kuzaliana kila mwaka.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha