Guterres asisitiza maendeleo kama njia ya matumaini kwenye kikao cha Baraza la Usalama (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 21, 2023
Guterres asisitiza maendeleo kama njia ya matumaini kwenye kikao cha Baraza la Usalama
Wajumbe wakihudhuria mjadala wa wazi wa Baraza la Usalama kuhusu kuhimiza amani endelevu kupitia maendeleo ya pamoja kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Novemba 20, 2023. (Eskinder Debebe/Picha ya UN/ Xinhua)

UMOJA WA MATAIFA - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesisitiza umuhimu wa maendeleo Jumatatu na kutoa shukrani kwa China kuandaa mjadala kuhusu suala hili muhimu katika Baraza la Usalama.

"Maendeleo ya binadamu yanaangazia njia ya matumaini - kuhimiza kinga, usalama na amani. Hii ndiyo sababu ya kuendeleza amani kunaendana sambamba na kuendeleza maendeleo endelevu na jumuishi," Guterres ameliambia Baraza la Usalama kwenye mjadala wa wazi juu ya kuhimiza amani endelevu kupitia maendeleo ya pamoja.

“Naishukuru Serikali ya China kwa kuitisha mjadala huu kuhusu uhusiano muhimu kati ya maendeleo na kudumisha amani,” amesema Guterres.

Ameendelea kusema kuwa maendeleo yenyewe hayatoshi kupata amani, na kuongeza kuwa hakuna amani iliyo salama bila maendeleo jumuishi na endelevu.

"Na hakuna janga kubwa kama kushindwa kuzuia migogoro. Ni kweli, mafanikio ya maendeleo mara nyingi ni miongoni mwa waathirika wa kwanza wa vita," Guterres ameongeza.

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kadiri nchi inavyokaribia kwenye migogoro, ndivyo inavyokuwa mbali na maendeleo endelevu na jumuishi.

"Nchi tisa kati ya kumi zenye Viashiria vya chini zaidi vya Maendeleo ya Binadamu zimekumbwa na migogoro au ghasia katika kipindi cha miaka kumi iliyopita," amebainisha.

"Kukosekana kwa usawa na ukosefu wa fursa, kazi za staha na uhuru vinaweza kuleta mfadhaiko na kuibua hali ya vurugu na ukosefu wa utulivu," ameongeza.

Kama ilivyoelezwa na Zhang Jun, mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa, kwenye mkutano na waandishi wa habari wa uliofanyika Novemba 1 juu ya mpango wa kazi wa kila mwezi, China imechagua kuandaa mjadala huo kuwa ni shughulikuu ikiwa nchi mwenyekiti wa baraza hilo Mwezi Novemba, kunaendana na nia yake ya kufuatilia chanzo cha migogoro duniani mwezi huu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha