Mabaki ya wanajeshi 25 wa China waliouawa katika Vita vya Korea yawekwa kwenye jeneza nchini Korea Kusini (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 23, 2023
Mabaki ya wanajeshi 25 wa China waliouawa katika Vita vya Korea yawekwa kwenye jeneza nchini Korea Kusini
Mabaki ya wanajeshi wa China waliouawa katika Vita vya Korea vya 1950-1953 yakiwekwa kwenye jeneza mjini Incheon, Korea Kusini, Novemba 22, 2023. (Xinhua/Yao Qilin)

INCHEON, Korea Kusini - Mabaki ya wanajeshi 25 wa China waliouawa katika Vita vya Korea vya Mwaka 1950-1953 yamewekwa kwenye jeneza nchini Korea Kusini siku ya Jumatano ili kurejeshwa katika nchi yao ya China ambapo hafla ya kuweka mabaki ya miili ya wanajeshi hao kwenye majeneza imefanyika mjini Incheon, Magharibi mwa Seoul, mji mkuu wa Korea Kusini.

Ujumbe wa China ukiongozwa na Naibu Waziri wa Masuala ya Wanajeshi Wastaafu Chang Zhengguo, maofisa wa Ubalozi wa China nchini Korea Kusini, wawakilishi wa wanafunzi wa China na kampuni za China nchini Korea Kusini pamoja na maofisa wa Wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini na wafanyakazi waliohusika na uchimbuaji na utambuzi wa mabaki hayo walihudhuria hafla hiyo.

Kikapu cha maua kiliwekwa kwenye makazi ya muda kwa ajili ya mabaki ya mashujaa wa Jeshi la Kujitolea la watu wa China (CPV). Chang alikwenda mbele kupanga kikapu cha maua na utepe.

Watu wote wa ujumbe wa China waliinama mara tatu kutoa heshima kwa mashujaa wa CPV na kuwasilisha maua. Upande wa Korea Kusini uliweka mabaki kwenye majeneza baada ya shughuli ya kumbukumbu ya upande wa China.

Tangu Mwaka 2014, China na Korea Kusini zimefanikiwa kukabidhi mabaki ya mashujaa 913 wa CPV nchini Korea Kusini kwa miaka tisa mfululizo, kwa kufuata kanuni za kibinadamu na kufanya ushirikiano wa kirafiki na wa kvivitendo.

Hafla ya mwaka huu ya kurejesha nyumbani mabaki ya mabaki ya CPV, ambayo ni ya kumi ya aina yake, imepangwa kufanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Incheon leo Alhamisi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha