Serikali ya Kenya, Mashirika ya Misaada yaharakisha misaada huku idadi ya vifo katika mafuriko ya maji ikifikia 71 (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 24, 2023
Serikali ya Kenya, Mashirika ya Misaada yaharakisha misaada huku idadi ya vifo katika mafuriko ya maji ikifikia 71
Watu wakitembea kupita njia iliyofurika maji baada ya mvua kubwa kunyesha katika Kaunti ya Garissa, Kaskazini mwa Kenya, Novemba 22, 2023. (Picha na Joy Nabukewa/Xinhua)

Serikali ya Kenya na mashirika ya misaada ya kibinadamu yanaharakisha kasi ya utoaji misaada ya kibinadamu huku mvua kubwa iliyonyesha ikiwa imeua watu 71 nchini kote Kenya.

Kwa mujibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya, kwa uchache watu zaidi ya 71 wamefariki, huku wengine zaidi ya 200 wakijeruhiwa na wengine zaidi ya 150,000 wamelazimika kukimbia maskani zao nchini kote Kenya, wakati mvua kubwa ikiendelea kunyesha na kusababisha maafa.

“Washirika wa misaada ya kibinadamu wanashirikiana na serikali kukabiliana na mafuriko ya maji na hadi sasa wamefikisha msaada wa chakula kwa watu 950,000 hivi katika kaunti husika,” Ofisi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Uratibu wa Mambo ya Misaada ya Kibinadamu (OCHA) imesema Jumatano.

Mafuriko hayo ya maji ni hali nyingine ya mfululizo wa hali ya hewa isiyo ya kawaida katika miaka ya hivi karibuni kuikumba Kenya na kanda ya Pembe ya Afrika, ambako watoto na jamii wanajikuta katika mwisho hatari wa athari za tabianchi duniani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha