Barabara Kuu mpya ya China ya kuvuka bahari yafikia hatua ya mwisho kukamilika (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 29, 2023
Barabara Kuu mpya ya China ya kuvuka bahari yafikia hatua ya mwisho kukamilika
Wajenzi wakifanya kazi kwenye handaki chini ya bahari la Barabara Kuu unganishi ya Shenzhen-Zhongshan katika Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China. (Xinhua/Deng Hua)

GUANGZHOU - Mradi wa barabara kuu ya kuvuka bahari kati ya miji ya Shenzhen na Zhongshan katika Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China uko hatua ya mwisho kukamilika baada ya umwagaji wa mwisho wa zege kukamilika siku ya Jumanne, huku kazi kwenye handaki la mviringo chini ya maji baharini lenye urefu wa karibu kilomita 6.8, likikaribia kukamilika ujenzi wake, imesema Kampuni ya Mawasiliano ya Mkoa wa huo wa Guangdong.

Handaki hilo ni sehemu ya barabara kuu yenye urefu wa kilomita 24 inayounganisha miji ya Shenzhen na Zhongshan, iliyo katika kila upande wa Mlango wa Mto Pearl.

Barabara hiyo kiunganishi cha miji ya Shenzhen-Zhongshan ni mradi muhimu wa kituo cha usafiri katika Eneo la Ghuba Kuu ya Guangdong-Hong Kong-Macao. Inajumuisha handaki moja la chini ya maji, madaraja mawili na visiwa viwili bandia, na kuifanya kuwa mojawapo ya miradi yenye changamoto zaidi ya barabara za kuvuka bahari duniani.

Barabara hiyo imepangwa kufunguliwa kwa matumizi ya umma Mwaka 2024. Mara tu itakapoanza kufanya kazi, muda wa kusafiri kati ya Shenzhen na Zhongshan utapunguzwa kutoka saa mbili hadi takriban dakika 20.

Barabara hiyo ya Shenzhen-Zhongshan, pamoja na miundombinu iliyopo kama vile Daraja la Hong Kong-Zhuhai-Macao, itaunda mtandao wa barabara za kuvuka bahari na mito katika Eneo la Ghuba Kuu, na kuongeza muunganisho wa miji, amesema Deng Xiaohua, Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Mkoa wa Guangdong.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha