Ngoma ya kijadi ya Simba yaingia kwenye madarasa ya shule ya msingi Zhejiang, China (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 30, 2023
Ngoma ya kijadi ya Simba yaingia kwenye madarasa ya shule ya msingi Zhejiang, China
Kocha Tong Panfeng akifundisha wanafunzi kufanya mazoezi ya vitendo ya ngoma ya kijadi ya simba ya China kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Kati ya Qiantong. (Picha na Zhang Yongtao/People’s Daily Online)

Kocha Tong Panfeng alifundisha wanafunzi kufanya mazoezi ya vitendo ya ngoma ya kijadi ya simba ya China hivi karibuni kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Kati ya Qiantong katika Wilaya ya Ninghai iliyoko Mji wa Ningbo, Mkoa wa Zhejiang, China.

Katika miaka ya hivi karibuni, shule hiyo imeanzisha madarasa ya kufundisha kwa njia ya ana kwa ana ngoma ya kijadi ya simba ya China, ili kuamsha ari ya utamaduni wa jadi kwenye madarasa, na kuwezesha watoto na vijana zaidi kujikita kwa kina katika burudani ya utamaduni wa jadi na kustawisha maisha ya shuleni.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha