Toleo la Mwaka wa Dragoni wa jadi wa China la maskoti wa Michezo ya Olimpiki, Bing Dwen Dwen lazinduliwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 30, 2023
Toleo la Mwaka wa Dragoni wa jadi wa China la maskoti wa Michezo ya Olimpiki, Bing Dwen Dwen lazinduliwa
Picha hii ya Novemba 29, 2023 ikionyesha toleo la Dragoni wa Mwaka Mpya wa Kijadi wa China la maskoti maarufu wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing na bidhaa zinazohusiana zenye leseni. (Xinhua)

BEIJING - Toleo la mwaka wa Dragoni wa kaleda ya kilimo ya China la maskoti wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, Bing Dwen Dwen lililotengenezwa maalum kwa ajili ya kusheherekea maadhimisho ya mwaka wa pili tangu kufanyika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing na Mwaka mpya ujao wa Jadi wa China unaowakilishwa na mnyama Dragoni utakaosheherekewa Mwezi Februari, Mwaka 2024 limezinduliwa kwenye Uwanja wa Taifa wa China siku ya Jumatano.

"Dragoni huyo anawakilisha roho ya Taifa la China na kutakia kila la kheri kwa afya na ustawi, ambayo inaendana na mshikamano uliosisitizwa na familia ya Olimpiki," Lin Cunzhen, mbunifu wa toleo hilo la Dragoni la Bing Dwen Dwen amesema.

Bidhaa zilizopewa leseni za toleo hilo jipya, amabzo ni pamoja na midoli, beji na vishikizio vya funguo, zitaingia sokoni Desemba 7.

"Jumuiya ya kimataifa inatarajia kuona urithi wa kitamaduni wa Olimpiki ukiendelea kung'aa duniani kote. China tayari imepata mafanikio katika kustawisha nguvu ya maskoti wa Olimpiki kupitia wanyama wanaowakilisha mwaka wa Jadi wa China na Sikukuu ya Mwaka mpya huo wa jadi” ameeleza Lin.

Wakati wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, ambayo iliambatana na Mwaka Mpya wa Jadi wa China Mwaka 2022, waandaaji walitoa toleo maalum la mwaka mpya huo la Maskoti Bing Dwen Dwen wakiwa wamevalia vazi lililokuwa na vitu vya simbamarara kusherehekea Mwaka Mpya wa Kijadi wa China wa Simbamarara.

"Watu daima wana hamu ya kutaka kujua mwonekano mpya wa Bing Dwen Dwen, kama sote tunavyojua jinsi alivyokuwa maarufu tangu kufunguliwa kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing karibu miaka miwili iliyopita," ameongeza, huku akibainisha kuwa watu wa China wana hamu ya kuona toleo jipya la baadaye la Bing Dwen Dwen litaonekanaje.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha